Wednesday, January 20, 2016

CHF YAKUBALIKA KAMA SULUHISHO LA MATIBABU NYEGENDI MKOANI LINDI

Wananchi wa Kata ya Nyengedi Lindi wakimsikiliza Mh. Nawanda DC wa Lindi akiwaelimisha umuhimu wa CHF katika kampeni ya uhamasishaji unaofanywa na NHIF kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo
naw2
Mkuu wa wilaya ya Lindi Mh. Yahya  Nawanda  akiwasikiliza  akisikiliza kwa makini hoja za wana Nyengedi ili kupata mrejesho wa huduma za afya katika kata hiyo. wakati  alipokuwa akiwaelimisha kuhusu  umuhimu wa huduma za CHF katika kampeni ya uhamasishaji inayofanywa na NHIF kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo
naw3
Mkuu wa wilaya ya Lindi Mh. Yahya  Nawanda  akisisiztiza jambo wakati NHIF ilipozindua kampeni hizo katika wilaya ya Lindi mkoa wa Lindi kulia ni Mkuu wa mkoa huo Mh. Jordan Lugimbana na kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa na Eugine Mikongoti Mkurugenzi wa wa Huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania, NHIF
naw4
Wana Nyengedi wakipima ili kujua afya zao katika kampeni ya CHF.
naw5
Wanakijiji wa Nyengedi wakidunduliza fedha ili kufikisha mchango wa sh. 10,000 kwa kaya ili wajisajili na CHF baada ya kuhamasika.
…………………………………………………………………………………..
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kishirikiana na Halmashauri ya Lindi Vijijini wameendelea na kampeni ya uhamasishaji wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF katika kata ya Nyangedi.
Katika uhamasishaji huo uliongizwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Nawanda kaya 70 zilijiunga papo hapo kwa kuchangia Shilingi 10,000 kwa kaya hivyo jumla ya Shilingi 700,000 zilikusanywa.
Aidha Mh. Nawanda alimwagiza Mganga Mkuu wa Wilaya kuhakikisha hakuna upungufu wa dawa katika kituo hicho na endapo litatokea hilo wananchi wamjulishe mapema.
Pia aliwakumbusha maagizo ya Mkuu wa Mkoa kwamba wasiojiunga na CHF watalipia Sh. 10,000 kwa matibabu kila wanapoenda kutibiwa kama hawaoni umuhimu wa kuchangia 10,000 kwa kaya kwa mwaka mzima na wakatibiwa kwa kadi.
Alimaliza kwa kuwahimiza watu kufanya kazi kwa bidii ili waweze kutimiza mahitaji yao kama afya kwani fursa za uzalishaji zipo.
Uhamasishaji wa CHF unaendelea katika kata mbalimbali za Lindi katika wiki hìi na baada ya hapo katika Halmashauri mbalimbali nchini.

No comments: