NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI NA MADINI ATEMBELEA KITUO CHA JEMOLOJIA ARUSHA

NAIBU Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe ametembelea kituo cha Jemolojia jijini Arusha ambacho hutoa mafunzo ya Jemolojia yanayojumuisha ukataji na uchongaji wa madini ya vito na kuyaweka katika maumbile ya kuvutia.

Naibu Katibu Mkuu alitembelea kituo hicho na Ofisi za Madini jijini Arusha ili kuona shughuli mbalimbali zinazofanyika pamoja na kuzungumza na watumishi.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (wa Tatu kushoto) akiangalia mashine ya ukataji madini iliyopo katika kituo cha Jemolojia jijini Arusha.Aliyevaa shati jeupe ni Mratibu wa Kituo hicho, Mussa Shanyangi, wa kwanza kushoto ni Afisa Madini Mkazi Ofisi ya Madini ya Merelani, Mhandisi Henry Mditi na wa pili kushoto ni Kaimu Kamishna wa Madini nchini, Mhandisi Ally Samaje.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (wa kwanza kulia) akiangalia mwamba uliochongwa, kunakshiwa na kuwa katika umbo la mjusi wakati alipotembelea Kituo cha Jemolojia jijini Arusha ambacho hutoa mafunzo yanayojumuisha ukataji na uchongaji wa madini ya vito na kuyaweka katika maumbile ya kuvutia. Wengine katika picha ni Afisa Madini Mkazi Ofisi ya Madini ya Merelani Mhandisi Henry Mditi, (wa kwanza kushoto), Kaimu Kamishna wa Madini nchini, Mhandisi Ally Samaje (wa pili kushoto) na wa pili kulia ni Kamishna Msaidizi wa Madini- Uchumi na Biashara, Salim Salim.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (kulia) akionyeshwa moja ya mashine zinazotumika katika Kituo cha Jemolojia jijini Arusha katika ukataji na uchongaji wa madini ya vito na kuyaweka katika maumbile ya kuvutia. Anayemwonyesha mashine hiyo ni Mratibu wa Kituo hicho, Mussa Shanyangi.

Comments