Monday, January 11, 2016

TATIZO LA MAJI JIMBO LA NYAMAGANA MKOANI MWANZA LAMTESA MABULA.


Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula akifafanua jambo ofisini kwake.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Mbunge
wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula amesikitishwa na
baadhi ya wakazi wa jimbo hilo kukabiliwa na ukosefu wa Maji safi na salama
huku baadhi ya miradhi ya maji ikichukua muda mrefu bila utekelezaji wake
kukamilika kwa wakati.
Mabula ameelezea masikitiko yake baada ya
kupokea malalamiko kutoka kwa wakazi wa jimbo la Nyamagana, juu ya kukosa
huduma ya maji ya bomba licha ya jimbo hili kuzungukwa na ziwa Victoria.
Mabula
ambae alikuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza katika uongozi uliomalizika
mwishoni mwa mwaka jana, amebainisha kuwa ipo miradi ya maji ambayo bado
haijatekelezwa kutokana na serikali kushindwa kutoa pesa kwa wakati jambo
ambalo amesema kuwa atalisemea mara kwa mara katika vikao vya bunge lijalo ili
kufanikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.

No comments: