RAIS mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na watoto watatu wa marehemu Mhandisi Suleiman Said Suleiman, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Nchini, TAA, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Upanga jijini Dar es Salaam, jana Januari 19, 2016 kutoa mkono wa pole. Marehemu Suleiman alifariki Jumatatu Januari 18, 2016 wakati akifanya mazoezi ya kuogelea kwenye bahari ya hindi na tayari amezikwa.
(Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
……………………………………………………….
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
RAIS mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, jana Januari 19, 2016 amehani msiba wa aliyekuwa Mkurugezi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini,
marehemu Mhandisi Suleiman Said Suleiman.
Dkt. Kikwete aliwasili nyumbani kwa marehemu Upanga jijini Dar es Salaam, akifuatana
na mkewe Mama Salma Kikwete majira ya saa 10;30, akitokea kijijini kwake Msoga mkoani Pwani.
Baada ya kuwasili, nyumbani kwa marehemu Rais mstaafu alipokewa na mdogo wa marehemu, Mhandisi, Nasiri Said Suleiman, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw. Laurent Mwigune, Mkurugenzi wa Sheria na Mawasiliano ya umma, Bw. Ramadhan Maleta, maafisa wa TAA, na wanafamilia wengine na kwenda moja kwa moja kuweka saini kitabu cha maombolezo.
Baada ya kufanya mazungumzo kwa muda, Watoto wawili wa marehemu ambao wanasoma nje ya nchi nao waliwasili na kupata fursa ya kusalimiana na Rais mstaafu, Dkt. Kikwete.
Watoto hao ni pamoja na motto mkubwa wa marehemu, Mohammed Said Suleiman, na mdogo wake Said Suleiman Said.
Baadaye Rais alikwenda kusaliamiana na mama mzazi wa marehemu, mke wa marehemu na
wafiwa wengine na kisha yeye na msafara wake kuondoka majira ya saa 11 jioni.
Mhandisi Suleiman Said Suleima, alifariki dunia Januari 18, 2016 majira ya asubuhi
wakati akifanya mazoezi ya kuogelea kwenye Bahari ya Hindi katikati ya Magogoni
na Kigamboni na kuzikwa jioni ya siku hiyo hiyo. Marehemu ameacha mjane na watoto watatu, Mohammed, Said na Hosam.
Akisaini kitabu cha maombolezo.
JK akisalimiana na Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa TAA, Bw. Ramadhan Maleta
JK akimpa pole mtoto wa mwishi wa marehemu, Hosam Suleiman Said Suleiman
JK akimpa pole mtoto mkubwa wa marehemu, Moahmmed Suleiman Said Suleiman
JK akimsikiliza Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini, TAA, Bw.Laurent Mwigune
JK akisalimiana na mdogo wa marehemu, Mhandisi Nasiri Said Suleiman
JK akimpa pole mama wa marehemu
Mama Salma Kikwete, akitoka nyumbani kwa marehemu Mhandisi Suleiman Said, baada ya kuhani msiba wake Januari 19, 2016
JK akisalimiana na Mkurugenzi wa Kazi Maalum wa TAA, Mhandis Thomas Junior Haule
JK akisalimiana na Meneja Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Mohamed R.Ally
Comments