WIZARA YA HABARI,UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA WAJASIRIAMALI WA KAZI ZA SANAA

BST1
Kaimu Mkurugenzi Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi.Leah Kihimbi akiongea na wajasiriamali wa kazi za Sanaa wa Mikono Cultural Heritage Ltd walipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.Bi leah aliwahaidi wasanii hao kufanya nao kazi kwa karibu na kuwapa ushirikiano mkubwa katika kazi zao.
BST2
Mwenyekiti wa kikundi cha wajasiriamali wa kazi za Sanaa Bw.Henry  Clemens (kushoto) akimweleza jambo Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Leah Kihimbi (kulia).Bw.Clemens aliomba serikali kuwawezesha kupata wawekezaji, na pia shughuli za za Sanaa ziwe rasmi ili wajipate kipato na kutengeneza ajira kwani wazalishaji wa Sanaa wanafiki milioni 3 kwa sasa.
BST3
Mwenyekiti wa kikundi cha wajasiriamali wa kazi za Sanaa Bw.Henry  Clemens akiishukuru serikali kwa kuonyesha nia ya kuwasaidia kwa kuanzisha Idara ya Sanaa na ivyo wataitumia kuimarisha kazi zao ili ziwanufaishe.Pembeni yake ni makamu mwenyekiti wa Kikundi icho Bw.Chief Eliewaha Shogholo Challi.
BST4
Baadhi ya wajasiriamali wa kazi za Sanaa wa Mikono Cultural Heritage Ltd wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bi leah kihimbi (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam
BST5
Picha ya pamoja.
Picha zote na Daudi Manongi-WHUSM

Comments