Thursday, January 14, 2016

MHE. KAIRUKI AAGIZA TATHMINI YA MAFUNZO YANAYOTOLEWA KWA WATUMISHI WA UMMA IFANYIKE

SONY DSCWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboje alipoitembelea taasisi hiyo mapema leo. 
SONY DSCWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa Taasisi ya Uongozi alipoitembelea taasisi hiyo mapema leo.  
SONY DSCWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akiwa katika kikao kazi na watumishi wa Taasisi ya Uongozi mapema leo. 
SONY DSC
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (mstari wa mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi ya Uongozi alipoitembelea taasisi hiyo mapema leo.  
……………………………………………………
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ameielekeza Taasisi ya Uongozi kufanya tathmini ya fursa za mafunzo zinazotolewa kwa Watumishi wa Umma kama zinakidhi mahitaji ya nchi.
Waziri Kairuki alisema hayo leo alipokutana na Watumishi wa taasisi hiyo jijini Dar es salaam.
“Mafunzo yanayohudhuriwa na Watumishi wa Umm kwa mahitaji yetu”elekezaWazirinakuongeza niKairukijambolamsingi alikuainisha
maeneo yanayohitaji kuboreshwa katika eneo la kujenga uwezo ili kufikia malengo.
Waziri Kairuki alisisitiza kuwa tafiti katika maeneo ya utoaji huduma kwa upande wa sekta ya umma zipewe msukumo na mapungufu yatakayobainika baada ya tafiti kukamilika yaelezwe bayana ili kupata kupata mrejesho.
Kwa upande wa viongozi wa umma Mhe. Kairuki alisema ni vema wapate mafunzo katika masuala mtambuka ili wafanye kazi kwa taratibu zilizowekwa.
Taasisi ya Uongozi, pamoja na masuala mengine huendesha Programu za mafunzo kutokana na mapungufu yanayoonekena kupitia tafiti mbalimbali zinazofanyika.
Taasisi ya Uongozi ilianzishwa kwa ushirikiano baina ya Serikali za Tanzania na Finland na kutangazwa katika gazeti la serikali la Tarehe 30 Juni, 2010.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Kny:KATIBU MKUU (UTUMISHI)

No comments: