Thursday, January 07, 2016

RAIS DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

ya1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli
akimkaribisha Rais Mstaafu wa Awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu
jijini Dar es Salaam.
ya2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  Ikulu
jijini Dar es Salaam leo Januari 6, 2016.
PICHA NA IKULU
………………………………………………………………………………………………..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amekutana na
kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Ikulu Jijini Dar es salaam jana Jumatano Januari 6, 2016.
Katika Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Kikwete amemtakia Rais Magufuli heri ya Mwaka mpya
na kumpongeza kwa uongozi mzuri.
Rais  mstaafu Kikwete pia amesema anaunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Rais
Magufuli ikiwemo ukusanyaji wa mapato ya serikali.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
06 Januari, 2016.

No comments: