Wednesday, January 06, 2016

AWAMU YA TATU YA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWAJILI YA KUMKOMBOA MWANAMKE WA KITANZANIA YAANZA DAR

 Washiriki wa Mafunzo hayo wakisikiliza kwa Makini Mafunzo hayo..
Awamu ya Tatu ya Mafunzo ya Ujarisiamali kwa Mkoa wa Dar es salaam yameanza leo. Wanawake 35 wa jiji la Dar es salaam Watanufaika na mafunzo ya ujasiriamali kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yanayoendeshwa na mtaalamu wa mambo ya Biashara Bw Felix Maganjila na Shekha Nasser. Mafunzo haya yenye lengo la kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuondokana na tatizo la ukossefu wa ajira kwa kujikita katika kujiajiri ndani ya Tasnia ya Urembo
 Mafunzo haya yamegawanywa katika awamu mbili ili kumsaidia mjasiriamali wa kike kujikwamua. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya Biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika Mpangilio wa Biashara ikiwemo Matumizi sahihi ya Rasilimali Muda, Fedha, Muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na Biashara yake
 Awamu ya Pili mshiriki anafundishwa Matumizi sahihi ya Vipodozi kuendana na wakati, mfano office makeup, day, evening na namna ya kumpamba bi Harusi. Pia wanafundishwa namna bora ya kutumia Vipodozi vya LuvTouch Manjano kwa lengo ya kuwa kila mshiriki atakayehitimu mafunzo haya aweze kujiajiri na kujitegemea kwa kuendesha maisha yake ya kila siku kwa kuwapambamba watu wenye Shuguli Mbalimbali
 Pamoja na mafunzo, kila mshiriki anaunganishwana Mwanamke mmoja mwenye mafanikio katika biashara au uongozi katika jamii kwa Lengo la kumuongoza katika safari yake ya biashara kwa muda wa mwaka mzima. Baada ya Wanawake hawa kuhitimu Mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa Mikopo kwajili ya kuwawezesha Kuanzisha Biashara wakiwa chini ya Uangalizi Maalum wa taasisi hiyo kwa Lengo la Kuhakikisha kila Mhitimu wa Mafunzo haya anapiga hatua na kuweza Kujitegemea.

No comments: