Wednesday, January 06, 2016

FASTJET KUZINDUA SAFARI KATI YA TANZANIA NA KENYA

Shirika la ndege la bei nafuu lapanua
wigo wa safari zake barani Afrika na kufungua safari ya kimataifa ya moja kwa
moja kutoka Nairobi kwenda Dar es Salaam na Kilimanjaro.
……………………………………………………………………………………………
 Fastjet imetangaza safari yake mpya ya kimataifa
ya kutoka Dar es Salaam kwenda Nairobi, Kenya kuwa itaanza rasmi mnamo tarehe
11 Januari 2016.
 
Fastjet imepewa ruhusa na serikali ya
Kenya kufanya safari zake nchini humo kufuatia makubaliano ya pamoja na mashirika
yanayotoa huduma za usafiri wa anga kati ya nchi hizi mbili za Tanzania na
Kenya, kama ilivyopitishwa na serikali ya Tanzania.
 
Vilevile Fastjet imetangaza kuwa
inatarajia kuzindua safari zake za anga kati ya Zanzibar na Nairobi na pia kati
ya Dar es Salaam na Mombasa ambapo uzinduzi huo utafanyika mapema mwaka huu
2016.
 
Tiketi za kurudi kutoka uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi kwenda uwanja wa ndege wa Mwalimu
Nyerere jijini Dar es Salaam na uwanja wa ndege wa Kilimanjaro zitakuwa za kila
siku mara tu baada ya uzinduzi huo na wasafiri watasafiri na ndege ya kisasa
aina ya  Airbus A319 ambayo hubeba abiria
156.
 
Kwa mujibu wa Fastjet, safari nyingine
za ndege zinatarajia kuzinduliwa kufuatia kuongezaka kwa maombi ya wateja wake
na hii ni kwa sababu ya unafuu wa bei zake sambamba na huduma bora.
 
Tiketi za safari hii mpya zimeanza
kuuzwa, na nauli za Nairobi/Dar es Salaam zitatozwa kwa $50 kwa safari moja, na
Dar es Salaam/ Nairobi zitatozwa kwa $80 kwa safari moja.
 
Nauli hizi ni pamoja na kodi ya
serikali  ambayo itachajiwa. Kwa mantiki
hiyo, Fastjet inawaomba abiria na wateja wake kwa ujumla kufanya booking mapema
iwezekanavyo ili kufaidika na bei nafuu ambayo hutozwa kuliko ndege zote ambazo
husafirisha abiria kati ya nchi hizi mbili.
 
“Usafiri wa anga katika uwanda wa Afrika
mashariki umekuwa na ushindani mkubwa
kutokana na safari nyingi bado hutoza nauli kubwa jambo linalosababisha
abiria wengi kushindwa kumudu safari hizo” alisema John Corse, Meneja Mkuu wa fastjet
kanda ya Tanzania.
 
“Wasafiri wengi wanaosafiri kati ya miji
hii miwili mikubwa yenye idadi ya watu wasiopungua milioni 8 hapa Afrika
Mashariki wamekuwa wakipatwa na vikazo mbalimbali vinavyowarudisha nyuma
kutokana na bei ya safari za ndege kuwa kubwa ambayo tunaamini imewakatisha tamaa
wasafiri wengi”, alisema Corse.
 
Matarajio ya Fastjet kufanya safari zake
nchini Kenya zitaleta matumaini mara tu baada ya shirika hilo kuzindua safari
hizo ambazo bei zake zimepokelewa na wateja wengi wanaosafiri na ndege zingine
hasa pale ambapo nauli za Fastjet zimepungua kwa asilimia 40 hivi.
 
“Jambo kuu la msingi ni kwamba ushindani
ni muhimu kwa wateja, kwa kuwa inampa mteja nafasi ya kuchangua unafuu wa nauli
atakayoimudu, na hali hii hufanya watalii na wajasiriamali na wageni
wanaotembelea nchi hizi mbili kuwa huru kuamua kwa raha kati ya Tanzania na
Kenya” Corse alisema.
 
“Hali
hii baadae italeta maendeleo ya pamoja kati ya nchi hizi mbili ambapo ukuwaji
wa biashara zao za ndani na nje, vilevile pia utalii utaimarika kwa kiasi
kikubwa na itakayo pelekea kukua kwa uchumi wa nchi hizi mbili”, aliongeza
Corse.
 
Pia
alisisitiza kuwa haileti maana halisi kwa mgeni ama mtalii kusafiri kwa zaidi
ya masaa 12 kutoka Dar es Salaam kwenda Nairobi Kenya na kumfanya achoke kama
ilivyo katika safari zingine. Na kwa kuwa sasa Fastjet imezindua safari mpya
kama hii ya nchi na nchi, basi inategemea wasafiri wengi watafaidika na huduma
za Fastjet.
Kwa
kuunga mkono mategemeo haya hapo baadae, hii ni baada ya Fastjet kufanya utafiti
wa kina na kubaini kuwa  abiria wake
waliweza kumudu bei zao na kuzikubali moja kwa moja.
 
Safari za kila siku za fastjet kutoka Dar
es Salaam zitaanza saa 3:50 asubuhi na kutua Nairobi-Kenya saa 5:10.
 
Safari za kurudi kutoka Nairobi kwenda
Dar es Salaam zitaanza saa 8:10 na kutua saa 10 :05 kulingana na saa za Afrika
mashariki.
 
Safari za kwenda Kilimanjaro kutoka Nairobi
zitaanza saa 5:10 na kutua saa 6:40 na safari ya kurudi kutoka Kilimanjaro
kwenda Nairobi zitaanza saa 7:10 na kutua saa 8: 40 kulingana na saa za Afrika
mashariki.
 
Fastjet inatoza nauli iliyo nafuu kadri
iwezekanavyo na kwa kutozingatia gharama za ushuru wa mizigo, vinywaji lakini
vyote hivi vinapatikana kama msafiri atagharamia kwa hiari yake mwenyewe.
 
Ukatishaji
tiketi mapema unaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kwa kupitia tovuti ya
festjet ambayo ni www.fastjet.com kupitia
kwa mawakala wa shirika hili, ama mteja anaweza kupiga simu Namba 0784 108900.
Malipo kwa ajili ya tiketi yanaweza kufanyika taslimu ama kwa kutumia benki ama
kwa njia ya mitandao ya simu za mikononi.
 
Fastjet imepanua wigo wa ofisi zake na
kwa sasa wanaendesha shughuli zao kimataifa kati ya Dar es Salaam ambako ndiyo
ofisi kuu na kushirikiana na Johannesburg Afrika Kusini, Lusaka-Zambia, Entebbe
– Uganda, Harare-Zimbabwe na Lilongwe nchini Malawi. fastjet pia hufanya safari
zake kwenda Entebbe.
fastjet pia hufanya safari zake za ndani
ya nchi kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro na pia kati ya Kilimanjaro
na Mwanza. Safari ya kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar itaanza tarehe 11th
Januari 2016.
Post a Comment