Monday, October 05, 2015

SIKU YA WANAFAMILIA YA KAMPUNI YA AIRTEL TANZANIA YAFANA DAR

 Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya AirtelTanzania wakishindana kucheza muziki chini ya bomba la mvua wakati wa bonanza la siku ya familia ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
 Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania 
wakifurahia michezo katika bwawa la kuogelea la Hoteli ya Kunduchi Beach
Wet in Wild, katika siku ya familia wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam
jana.
 Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania 
wakifurahia michezo ya bembea hafla ya siku ya familia ya kampuni hiyo
jijini Dar es Salaam jana.
 Baadhi ya wafanyakazi na wanafamilia wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania wakianza mashindano ya mbio za magari madogo yaendayo kasi ‘Go Kat’ katika maadhimisho ya siku ya wanafamilia hao jijini Dar es Salaam jana.
 Wafanyakazi na familia zao wakichukua chakula kwa pamoja kuonyesha 
upendo na mshikamano wao ambao pia ni sehemu ya mambo muhimu yanayochangia mafanikio kampuni yao.
 Mmoja wa watoto wa wafanyakazi wa Airtel akimpakulia mwenzake kama ishara ya upendo wakati wa siku ya wanafamilia wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kulia), akibadilishana mawazo na baadhi ya wa wafanyakazi wa kapuni hiyo katika maadhimisho ya siku ya wanafamilia wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.

  Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
Tanzania, Patrick Foya (kushoto) akimpomgeza Hagulwa Joseph,  mtoto aliyeshinda katika shindano la kusakata dansi lililofanyika kunogesha
bonanza la siku ya familia ya kampuni hiyo jijini Dar es Saalaam jana.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

WITO umetolewa kwa wafanyakazi nchini kushiriki michezo kwani kwa 
kufanya hivyo kutaweza kuimairisha afya zao hivyo kuongeza ufanisi
mahali pao pa kazi.

Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya
 
Simu za Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania, Jane Matinde wakati wa
bonanza la kila mwaka la siku ya wanafamilia wa kampuni hiyo.

Bi Jane alisema michezo ni kichocheo muhimu katika afya ya mwili na
 
akili hivyo endapo wafanyakazi watashiriki katika shughuli za michezo
kutaifanya miili yao isiwe goigoi.

"Moja ya mambo muhimu katika maendeleo mahali pa kazi ni bila shaka ni
 
kuwa na  wafanyakazi wenye afya ya mwili na akili, sisi kama Airtel
Tanzania tunajali sana afya za wafanyakazi wetu," alisema.

Naye Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Airtel Tanzania, Patrick Foya
 
alisema ni desturi yao kuwa na siku maalumu kila mwaka ya
kuwakutanisha wafanyakazi wao na familia zao ili pamoja na kushiriki
michezo na mambo mengine ya kuburudisha nyoyo zao zao lakini pia
huitumia siku hiyo kuzidi kuimarisha mshikamano miongoni mwao.

"Umoja na mshikamano ni nyenzo muhimu mahali pa kazi, lakini pia
 
ukiwa na mfanyakazi anayetoka katika familia iliyokosa utulivu, lakini
pia mfanyakazi legelege hawezi kufanya kazi zake kwa ufanisi,"
akaongeza Bwana Foya.

Zaidi ya wafanyakazi na wanafamilia za 500 walishiriki katika bonanza
 
hilo na kushiriki michezo mbalimbali kama vile kucheza muziki,
kuvutaka kamba, soka la baharini, wavu na kuogelea.

No comments: