Thursday, October 01, 2015

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MERCK SADICK ANATARAJIWA KUWA MGENI RASMI KATIKA MKUTANO MKUU WA JUMUIYA YA WAISLAMU WA AHMADIYYA KUANZA KESHO



MKUU wa mkoa wa Dar es salaam Merck Sadick anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa mwaka  wa 46 wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Tanzania utakaofanyika kuanzia tarehe 2 hadi 4 octoba mwaka huu katika eneo la kitonga, Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaaM.

Hayo yamesemwa na Amir Mbashiri Mkuu Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Sheikh Tahir amesema kuwa lengo kuu la mkutano huo ni kukumbushana misingi sahihi ya dini tukufu ya Islam, kukuza udugu na urafiki miongoni mwa wanajumuiya na wananchi kwa ujumla na kuhamasisha amani katika jamii.

Ameongeza kuwa kwa muda wa miaka mitano Jumuiya imekuwa ikiandaa mikutano ya amani katika mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuhamasisha jamii, dini mbalimbali na asasi za kijamii kuishi kwa amani licha ya kuwepo kwa tofauti za itikadi na mitazamo.

Kwa uapande wake Katibu Mkuu waJumuiya hiyo Seif Hassan amesema kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, amewaasa viongozi wote wa dini tofauti kutojihusisha na mambo ya kisiasa na kushukuru ushirikiano mzuri wanaoupata kutoka serikalini katika kutekeleza shughuli na kutarajia kuwa serikali na wadau wengine kujitokeza kuendelea kuwaunga mkono katika shughuli zijazo.

Aidha Jumuiya inatoa huduma ya elimu ya sekondari katika mkoa wa Dar es salaam na shule ya msingi katika mkoa wa morogorona kupitia asasi ya Humanity First Jumuiya imetoa msaada wa vifaa tiba ikiwa ni pamoja na mashine ya kupimia saratani ya matiti (Mammogram) katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. 

Takribani washiriki 3500 kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo Kenya, Uganda, Burundi, Malawi, na Msumbiji watahudhuria katika mkutano huo uliobeba kauli mbiu isemayo “mapenzi kwa wote, chuki si kwa yeyote”

No comments: