Thursday, October 01, 2015

KILA JUMATATU YA KWANZA YA MWEZI OKTOBA NI SIKU YA MAKAZI DUNIANI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

 TAARIFA KWA UMMA
 Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inapenda kuwataarifu  Wananchi wote kwamba kila Jumatatu ya kwanza ya mwezi Oktoba ni Siku ya Makazi Duniani  ambayo huadhimishwa Duniani kote.

Nchini, mwaka huu tarehe 05/10/2015  –  Jumatatu, Maadhimisho ya siku hii yanategemewa kufanyika katika viwanja vya Karimjee kuanzia saa mbili na nusu asubuhi (2:30) mpaka saa nane mchana (8:00).

Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni; 
“Maeneo ya Umma kwa Wote”

Mgeni rasmi katika Maadhimisho haya anatarajiwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe.William Lukuvi.

“Wananchi wote mnakaribishwa”

Imetolewa na Katibu Mkuu

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

No comments:

KIKWETE ATEULIWA KUWA MWAKILISHI WA NGAZI YA JUU WA MWENYEKITI WA KAMISHENI YA AU

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), Mhe. Mahmoud Ali Youssouf, amemteua Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Ki...