Wednesday, October 07, 2015

MAKAMU WA RAIS AONGOZA WAOMBOLEZAJI KIFO CHA KAKA WA WAZIRI MEMBE

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili nyumbani kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (Mb) kumpa pole kufuatia kifo cha kaka yake Waziri Membe, Bw. Simon Kamillius Membe aliyefariki dunia siku chache zilizopita huko nchini India. 
Makamu wa Rais akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu, nyumbani kwa waziri Membe leo tarehe 06-10-2015.
Makamu wa Rais akiwapa pole familia ya Marehemu Simon Kamillius Membe aliyefariki dunia siku chache zilizopita huko nchini India. 
 Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamin Mkapa akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili nyumbani kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (Mb) kumpa pole kufuatia kifo cha kaka yake Waziri Membe, Bw. Simon Kamillius Membe aliyefariki dunia siku chache zilizopita huko nchini India. 

 Rais Mstaafu Mhe.Benjamin Mkapa akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu, nyumbani kwa waziri Membe leo tarehe 06-10-2015.
 Rais Mstaafu Mhe.Benjamin Mkapa akiwapa pole familia ya Marehemu Simon Kamillius Membe aliyefariki dunia siku chache zilizopita huko nchini India.

Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa marehemu.

Post a Comment