Monday, October 05, 2015

MAGUFULI AHUTUBIA WANANCHI WA KATESH ASUBUHI HII MKOANI MANYARA

 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika Viwanja vya Ofisi ya CCM mjini Katesh, mkoani Manyara mapema jana asubuhi .Dkt Magufuli anatarajia kuhutubia mkutano mkubwa jioni ya leo mjini Karatu unaotarajiwa kurushwa live na kituo cha Star TV.
 Kiongozi wa Kampeni za Mgombea Urais wa CCM,Ndugu Abdallah Bulembo akiwaonesha wananchi wa Katesh mfano wa karatasi ya kupigia kura na namna ya kumpigia kura Dkt Magufuli ifikapo Oktoba 25 mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu.
Mamia ya wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika Viwanja vya Ofisi ya CCM mjini Katesh, mkoani Manyara mapema jana asubuhi. Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hanang,Mama Mary Nagu akiwahutubia wananchi wa Katesh mapema jana asubuhi kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,uliofanyika katika uwanja wa CCM,mkoani Manyara.
 Mamia ya wananchi wakifuatila mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia mapema leo asubuhi kwenye Viwanja vya Ofisi ya CCM mjini Katesh, mkoani Manyara mapema jana asubuhi
Post a Comment