Tuesday, October 13, 2015

DK. JOHN POMBE MAGUFULI AMPONGEZA DIAMOND PLATNUMZ KWA KUNYAKUA TUZO TATU ZA MUZIKI NCHINI MAREKANI

????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mkoa wa Lindi kwenye mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya msingi Pilipili mjini Lindi wakati akiomba kumpigia kura za ndiyo ili aweze kuwatumikia watanzania kwa uadilifu mkubwa.
Akizungumza katika mkutano huo Dk. John Pombe Magufuli pamoja na mambo mengine amempongeza mwanamuziki Nassib Abdul (Diamond Platnumz ambaye amejishindia tuzo tatu za kimataifa baada ya kutwaa tuzo ya AFRIMMA 2014 moja wapo ikiwa ni ya  Msanii bora wa kiume Afrika Mashariki. zinazoandaliwa na kufanyika nchini Marekani.
Diamond Platnumz amejishindia tuzo hizo pamoja na wanamuziki wenzake wa kitanzania ambao kila mmoja amejishindia tuzo moja kila mmoja  ambao ni Ommy Dimpoz, Lina Sanga na Vanessa Mdee, Dk. Magufuli amesema atahakikisha nawaanzishia mfuko maalum wasanii na wanamichezo ili kulinda maslahi yao waweze kunufaika na kazi zao ambazo wamekuwa wakidhulumiwa kila wakati ukilinganisha na wenzao wa mataifa yaliyoendelea.
Dk. John Pombe Magufuli amempongeza mwanamuziki Diamond pia kwa kujitoa kwake na kumpigia kampeni wakati wote wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Tanzania zinazoendelea nchini kote,  ambapo uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unatarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu nchini kote ukishirikisha vyama mbalimbali vya siasa(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-LINDI)
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akiuhutubia umati wa wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wake wa kampeni mjini Lindi uliofanyika uwanja wa Pilipili mjini Lindi.
????????????????????????????????????
Umati wa wananchi waliojitokeza katika mkutano huo wakimsikiliza Dk. John Pombe Magufuli hayupo pichani wakati alipokuwa akihutubia.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Mgombea Ubunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo uliofanyika mjini Lindi na kumuombea kura Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimuombea kura Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano uliofanyika mjini Lindi leo.
????????????????????????????????????
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na aliyekuwa mgombea Urais ndani ya Chama cha Mapinduzi Mh. Bernald Membe akimuombea kura Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Lindi leo.
????????????????????????????????????
Mwenyekiti wa CCM mkoani Lindi Mzee Ali Mtopa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Alhaji Abdallah Bulembo wakicheza wimbo wa Mbele kwa mbele uliokuwa ukitumbuizwa na kundi la TOT katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mwanamuziki Ali Kiba akitumbuiza katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Ali Kiba na kundi lake wakifanya makubwa zaidi katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli Mama Salma Kikwete wakiwa wamekaa meza kuu pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo kulia ni Mgombea ubunge wa jimbo la Mtama Nape Nnauye na kutoka kushoto ni Mh. Bernald Membe na Mgombea Ubunge wa jimbo la Lindi mjini Hassan Selemani Kaunje. 
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akimpongeza Mh. Bernald Membe mara baada ya kumuombea kura kwenye mkutano huo. 
????????????????????????????????????
Yamoto Bandi wakikamua jukwaani.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Mama Salma Kikwete  wakati wakiwa kwenye mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akimpongeza Mke wa Rais Mama Salma Kikwete mara baada ya kumpigia debe leo katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Lindi.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akimpigia debe mgombea ubunge wa jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika mjimbo la Mtama.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi kitabu cha Ilani ya Uchaguzi wakati alipomnadi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Mtama leo.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni jimbo la Mtama mkoani Lindi. 
????????????????????????????????????
Mwanamuziki Ali Kiba na kundi lake wakiburudhisha katika mkutano wa kampeni uliofanyika jimbo la Mtama mkoani Lindi.
????????????????????????????????????
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa akimkaribisha Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli ili zungumza na wananchi na kuomba kura katika jimbo la Mtama.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili katika mkutano huo huku akiongozana na mwenyeji wake mgombea ubunge wa jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi Mh. Kassim Majaliwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Ruangwa.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akionyesha Ilani ya Uchaguzi ya CCM wakati akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi Mh. Kassim Majaliwa.
????????????????????????????????????
Uwanja mzima ukiwa umetapakaa picha za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli mjini Ruangwa.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi mjini Nachingwea wakati akiomba kupigiwa kura za ndiyo katika uchaguzi mkuu ujao.
????????????????????????????????????
Umati wa wananchi ukiwa umefurikwa kwenye uwanja wa Sokoine mjini Nachingwea.
????????????????????????????????????
Nitajifunikwa ili nipate kivuli kutokana na jua kali lakini pia ujumbe utafika kwa wapiga kura.
????????????????????????????????????
Ujumbe mzito uliomo katika bango hili unafaa kufanyiwa kazi na wananchi.
Post a Comment