Thursday, October 08, 2015

BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA MADAWATI 200 KWA SHULE YA MSINGI BUYUNI ILALA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto) akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 200 kwa Shule ya Msingi Buyuni iliyopo Chanika katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Benki hiyo tawi la Kariakoo, Andrew Augustine, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Asha Mapunda (wa pili kulia) na Mkuu wa shule hiyo, Maulidi Maliki.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Shule Buyuni, Maulidi Maliki, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Asha Mapunda na Meneja wa Benki wa Benki ya CRDB tawi la Kariakoo, Andrew Augustine wakipiga makofi baada ya Benki ya CRDB kukabidhi msaada wa madawati 200
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkabidhi keki ya maalum ya shukrani Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Asha Mapunda wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charle Kimei (kushoto), akikagua sehemu ya madawati 200 yaliyokabidhiwa na Benki ya CRDB kwa uongozi wa Shule ya Msingi Buyuni. Kulia ni Meneja wa Benki hiyo tawi la Kariakoo, Andrew Augustine. 

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza katika hafla ya kukabidhi madawati 200 kwa Shule ya Msingi Buyuni iliyopo ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. Madawati hayo yametolewa na Benki ya CRDB ili kukabiliana na upungufu wa madawati shuleni hapo.


Post a Comment