Monday, January 04, 2016

NAIBU WAZIRI KIGWANGALA ATEMBELEA MNH AAGIZA KUBORESHWA HUDUMA ZA KULIPIA.

images (9)
Naibu Waziri wa Afya , maendeleo ya jamii, jinsia , wazee na watoto Dokta Khamis Kigwangwala leo ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili  -MNH- na kuagiza uongozi wa hospitali hiyo kuboresha huduma za kulipia kwa kiwango cha daraja la kwanza ili kuongeza mapato ya hospitali na pia mgonjwa aweze kuona thamani ya pesa yake.
Akizungumza mara baada ya kutembelea hospitali hiyo ikiwemo Idara  ya magonjwa ya dharura na ajali  pamoja na mashine za CT  Scan na MRI , Dokta Kigwangala amesema watumishi wa MNH   hawanabudi kuwa wabunifu ili kuhakikisha huduma zinazotolewa zina kuwa bora zaidi na zenye faida .
“ Hospitali ya Taifa Muhimbili  ina madaktari  bingwa wengi  na wenye uwezo mkubwa wa kutoa huduma na wengine ni wataalam wa  magonjwa mbalimbali  ikiwemo  moyo na  figo hivyo naamini  wanaweza kufanya mabadiliko makubwa “ amesema Kigwangala .
Awali Mkuu wa Idara ya Mionzi Dokta Florah Lwakatare  amemueleza Naibu Waziri Kigwangala kwamba mashine ya mpya ya CT Scan ambayo imenunuliwa na serikali inaendelea na majaribio pamoja kuwapatia mafunzo watumishi wake kwakua kua mashine hiyo ni ya hali ya juu sana .
Amefafanua kuwa  mashine hiyo ya kisasa  inafanya kazi kwa haraka  na kwamba tangu ianze majaribio hapo  juzi mpaka leo tayari  wagonjwa 26 wameshapimwa .
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Profesa Lawrence Mseru amemuhakikishia  Naibu Waziri  kuwa  MNH itaendelea kutoa huduma bora za afya .

No comments: