Thursday, January 07, 2016

BILIONI 18.77 ZIMETUMWA KWENYE AKAUNTI ZA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI HAPA NCHINI.

 Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mipango akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Fedha zilizo pelekwa katika halmashauri zote hapa nchini kiasi cha shilingi bilioni 18.77  kwenye akaunti za shule za msingi na Sekondari kwaajili ya kutoa elimu bure kwa wanafuzi wa shule zote hapa nchini.
 Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Beno Nduru akifafanua jambo kwenye mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia Katibu Mkuu wa wizara ya Fedha na Mipango, Servacius Likwelile.
 Kaimu kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alfayo Kidata akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na ukusanyaji wa mapato katika Malaka ya Mapato Tanzania kwa kila robo mwaka. 
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mipango jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

KIASI cha shilingi bilioni 18.77 zimetumwa kwenye akaunti za shule za Msingi na Sekondari za halmashauri zote hapa nchini kwaajili ya wanafunzi kusoma bure.

Hayo yamesemwa na Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mipango wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Pesa hizo zimegawanywa kwenye akaunti za shule za shule za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote kiasi cha shilingi bilioni 15.7 na bilioni 3  kwenye akaunti vyombo vya usimamizi wa mitihani katika Halmashauri zote hapa nchini.

Dk.Mipango amewatahadharisha wakuu wa Mikoa, wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri zote kutumia ipasavyo pesa hizo kwa kuwa zikitumika kwa matumizi mengine watalala nao mbele kwa kula jasho la wananchi.

Pia Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Mipango amewaomba waalimu wakuu wa shule zote za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote hapa nchini waweke wazi matumizi ya fedha hizo  katika mbao za matangazo kwa kila shule ili kila mzazi aweze kujua kiasi gani kimetumika.

No comments: