Friday, October 02, 2015

WAFANYAKAZI WATAKIWA KUFUATILIA MAKATO YAO

Mkurugenzi wa Utafiti, Tathmini na Sera wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ansgar Mushi.

Na Mwandishi wetu, Dodoma
WANACHAMA wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii wametakiwa kufuatilia makato yao kwa kuwa baadhi ya waajiri wanachelewa kupeleka makato yao. 

Mbali na hilo, waajiri wa metakiwa kutowalazimisha wafanyakazi wao, kujiunga na mfuko wasio upenda badala yake wapewe nafasi ya kujieleza.Kauli hiyo, ilitolewa jana na Ofisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Kenneth Batanyita alipokuwa akitoa elimu kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi (TUCTA), mkoani Dodoma.

Mkurugenzi wa Utafiti, Tathmini na Sera kutoka SSRA, Ansgar Mushi aliwatoa hofu wanachama wa mifuko hiyo, ya jamii kwa madai kuwa haiwezi kufa.Katibu wa Chama cha Wafanyakazi, Mkoa wa Dodoma,Ramadhani Mwendwa aliwataka wafanyakazi kujenga hoja wanapodai stahiki zao badala ya kulalamika.
Post a Comment