Sunday, October 04, 2015

MCHUNGAJI MTIKILA AFARIKI DUNIA


 Gari alilokuwa Mchungaji Mtikila, dereva na mlinzi wake

Mwenyekiti  wa  Chama  cha DP,Mchungaji Christopher Mtikila amepata ajali mbaya ya gari maeneo ya Chalinze na kufariki Dunia papo hapo.

Mtikila alikuwa na mlinzi na dereva na yeye Mtikila amefia pale pale na wengineo hali zao ni mbaya na kuwahishwa katika hospitali ya Tumbi.

RPC wa Pwani amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo eneo la Msolwa.

Mwili wa Mchungaji Mtikila umehifadhiwa hospitali ya Tumbi. Mwenyezi Mungu ampe mwanga wa milele. Amen!!

Post a Comment