Tuesday, October 06, 2015

DK. JOHN POMBE MAGUFULI: NAMKUBALI SANA DK. WILBROAD SLAA NI MPIGANAJI WA KWELI VITA YA MAFISADI

????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi  kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Bwawani mjini Karatu mkoani Arusha wakati akiwaomba wananchi wa mji huo kumpigia  kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika nchini kote na kushirikisha vyama mbalimbali vya kisiasa.
Dk. John Pombe Magufuli amewaambia wananchi hao kwamba anampenda na kumkubali sana Dk. Wilbroard Slaa kwa sababu ni mtu mkweli, mwaminifu, mchapakazi na mtu ambaye yuko tayari kupambana na ufisadi kwa uwazi na mtu aliyewapenda watu wake wa Karatu na Watanzania kuwa ujumla kutokana na jinsi alivyopigania haki za watu hasa katika masuala ya ubadhirifu wa mali ya Umma na kuwatetea watanzania walio masikini.
Amewaomba wananchi hao kumchagua yeye kwa sababu kwake ni Kazi Tu na akifanikiwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakuwa rais wa watanzania wote bila kujali Itikadi zao za kisiasa, Makabila yao wala dini zao lakini pia atakuwa rais wa watanzania wasiokuwa na vyama wala dini na kuwatumikia kwa haki huku akimtanguliza mungu mbele.
Dk John Pombe Magufuli leo amefanya mikutano mbalimbali katika wilaya za Hanang, Hydom, Mbulu  na Karatu  huku akikutana na wananchi mbalimbali waliokuwa wakimsimamisha ili kusalimiana naye katika maeneo mbalimbali aliyopitia akitokea Hangan mkoani Manyara kuelekea Karatu mkoani Arusha. (PICHA NA JOHN BUKUKU- FULLSHANGWE-KARATU)
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi  kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Bwawani wilayani Karatu mkoani Arusha jana.
????????????????????????????????????
Maelfu ya wananchi wakiwa katika mkutano huo uliofanyika mjini Karatu jana.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akicheza muziki na wasanii mbalimbali wakiwemo wa Kundi la TMK Family Chege na Temba  kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Bwawani mjini Karatu  jana.
????????????????????????????????????
Full Nyomi kama inavyoonekana.
????????????????????????????????????
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ngorongoro Michael Lekule Laizer akizungumza jambo na Mgombea ubunge wa jimbo la Hanang Dk. Mary Nagu katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Wananchi waliohudhuria katika mkutano huo wanynyanyua mikono yao juu na kuimba wimbo wa Alinserema unaopendwa na kuimbwa mara nyingi na Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Karatu Dk. Roli.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea ubunge na udiwani wa Karatu kulia ni Dk Roli na kushoto ni Ndugu Ali  mgombea udiwani Karatu.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea ubunge wa mkoa wa Arusha , kutoka kulia ni  wagombea wa viti maalum Arusha Viola Mfuko, Catherin Magige na Dk. Roli.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo wakinyoosha mikono yao juu kama ishara ya kukubali maneno ya Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Sasa ni wakati wa Burudani.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wagombea ubunge wa mikoa ya Manyara na Arusha wakishiriki kucheza muziki wa kizazi kipya ilioburudiswa na kundi la TMK Family.
????????????????????????????????????
Kulikuwa na mabango yenye ujumbe  mbalimbali wa kumsifia Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba yake.
????????????????????????????????????
Hapa Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wakati akiwa njiani kuelekea wilayani Karatu.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi  kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika mji wa Dongobesh mkoani Manyara.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano uliofanyika mjini Mbulu.
????????????????????????????????????
Mamia ya wananchi wa mji wa Mbulu mkoani Manyara wakimsikiliza Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Baadhi ya vijana waendesha bodaboda wakipata sera.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi waliokuwa na mabango yaliyoelezea shida zao wakiwa katika mkutano wa kampeni katika mji wa Dongobesh mkoani Manyara wakiwasilisha ujumbe wao Dk. John Pombe Magufuli aliyapokea na kuyachukua mabango yao ili kufuatilia kero zao mara atakapochaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Mbulu vijijini Ndugu Fratei Gregory Massay mjini Hydom.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wakifurahia jambo wakati walipokuwa wakisikiliza hotuba ya Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkuatno wa kampeni uliofanyika mjini Katesh wilayani Hanang.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Hangan Dk Mary Nagu katika kutano wa kampeni uliofanyika mjini Katesh wilaya ya Hanang.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimsikiliza  mgombea ubunge wa jimbo la Hanang Dk. Mary Nagu katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Katesh  jana.
Post a Comment