Saturday, September 05, 2015

WAZIRI WA KAZI NA AJIRA, GAUDENTIA KABAKA, AZINDUA BODI YA WADHAMINI MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, WCF


 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, (kulia), akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha Mshomba, wakati wakichukua nafasi zao kwenye uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, jijini Dar es Salaam, Septemba 4, 2015. Waziri Kabaka alizindua bodi hiyo itakayoongozwa na Mwenyekiti wake,   Bw. Emmanuel Humba

 Waziri Kabaka akitoa hotuba ya uzinduzi wa Bodi hiyo

 Mwenyelkiti wa Bodi ya Wadhamini Bw. Emmanuel Humba akipokea chati cha usajili wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Kutoka kwa Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudentia Kabaka (Cheti cha Usajili kimetolewa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Nchini SSRA)
 Mwenyekiti wa Bodi, Bw. Humba, (katikati), akitoa hotuba yake. Kulia ni Waziri Kabaka na kushoto ni Mkurugeniz Mkuu, WCF, Masha Mshomba
 Mgeni rasmi, Waziri Kabaka, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya wadhamini ya Mfuko huo, baada ya uzinduzi rasmi wa bodi
 Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudentia Kabaka akitoa hotuba kwa Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) pamoja na wageni waalikwa kabla ya kuzindua Bodi hiyo Rasmi.Post a Comment