Friday, September 11, 2015

RAIS KIKWETE APOKEA TUZO YA UTAWALA BORA

 Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Asha Rose Migiro akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Tuzo maalum ya “Africa Achiever’s Award in The Category of Good governance in Africa,” wakati wa hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam jana. Dkt.Migiro alimwakilisha Rais Kikwete katika hafla ya kutunukiwa Tuzo hiyo huko Afrika ya Kusini hivi karibuni.
 Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Asha Rose Migiro akisoma ujumbe maalum uliombatana na tuzo muda mfupi kabla ya kuikabidhi Tuzo hiyo kwa Rais Kikwete.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba fupi baada ya kupokea TuAfrica Achiever’s Award in the Category of Good Governance in Africa,” kutoka kwa Waziri wa katiba na Sheria Dkt.Asha Rose Migiro aliyeipokea kwa niaba ya Rais huko Afrika ya Kusini.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Asha Rose Migiro aliyekabidhi Tuzo kwa Rais(Watatu kushoto),Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(Wapili kushoto), Wamasheria Mkuu wa Serikali Mh.George Masaju(wapili kulia), Mwenyekiti wa Tume ya Haki Za Binadamu Mhe.Tom Nyanduga(kulia) na Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mh.Suzan Mlawi(kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya Dkt.Migiro Kumkabidhi Rais Kikwete Tuzo ya “ Africa Achiever’s Award in the Category of Good Governance in Africa” ikulu jijini Dar es Salaam jana (picha na Freddy Maro)

Post a Comment