Thursday, September 10, 2015

KATIBU MKUU WA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA AFUNGUA MAONYESHO YA BIASHARA YA BIDHAA ZA CHINA 2015, DAR ES SALAAM LEO


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Uledi Mussa (wa tano kulia), akifurahi baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi wa Maonyesho ya Biashara ya Bidhaa za China 2015, uliofanyika Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam leo asubuhi. Wengine na maofisa biashara wa China na wadau wa masuala ya biashara.
 Hapa Katibu Uledi Mussa akitia saini wakati wa ufunguzi wa maonyesha hayo.
 Hapa akioneshwa bidhaa mbalimbali.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Uledi Mussa, akizungumza na wanahabari.

Na Dotto Mwaibale
SHIRIKA la Viwango Tanzania(TBS) limesema  bidhaa zinazotoka china zina ubora huku likitoa mwito kwa wafanyabishara kutumia fursa ya kujifunza kupitia maonesho ya bidhaa za china.

Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Joseph Masikitiko,Mkurugenzi wa biashara Agnes Mneney alisema haiwekani kujua kma bidhaa zina ubora au la kwa kuangalia kwa macho.

Alisema TBS ndio waliopewa dhamana na Serikali ya kukangua ubora wa bidhaa zote za ndani na za nje kisha kubainisha kwa wananchi kama bidhaa zina ubora au ni hafifu kwa maslahi ya taifa.
''TBS ndio imepewa dhamana ya kudhibiti bidhaa zenye ubora kwa maslahi ya taifa kwahiyo watanzania wasipende kutoa hukumu kwa njia ya kukaangali kwa macho,''alisema.

Agnes alisema mtanzania anachotakiwa kufanya ni kuhahakikisha ananunua bidhaa ambazo zina nembo ya TBS kwasababu bidhaa zote sokoni zinatakiwa kuwa na viwango vya shirika hilo.

''Bidhaa za nchini China lazima ziwe na vuwango vya ubora vinavyotolewa TBS ili kuzingatia kiwango cha ubora katika soko la Tanzania,''alisema.

Kwa upande wake Mwakilishi wa masuala ya biashara na uchuminchini China,Lin Zhiyong alisema maoyesho ni ya siku tatu ambapo zaidi ya wafanyabishara kutoka nchina 230 wameshawasili nchini.     

Akizungumzia ubora wa bidha zao,Zhiyong alisema kupitia udhibiti waTBS wafanyabishara wa china wameanza kuondoa bidhaa ambazo ni hafifu sokoni.

''Bidhaa hafifu zimeanza kuondolewa sokoni kwa takribani miezi mitatu iliyopita ili kuimarisha ushirikiano wetu na TBS  na mkakati wa wafanyabishara wa China ni kuhakikisha tunaondoa bidhaa zote hahifu ili kulinda bora,''alisema.

Kwa upende wake Katibu Mkuu wa viwanda na bishara,Uledi Mussa alisema Tanzania imekuwa na urafiki mkubwa wa masuala ya kiuchumi na China.

Alisema kupitia urafiki huo ni imani yake China itaisaidia Tanzania kujenga viwanda na kuisaidia Tanzania kuzalisha vitu vyenye ubora na kuviuza.

Mussa alisema Tanzania inaanda mpango wa kuanzisha viwandana kwamba dhamira ya wizara husika ni kuwawesha wafanyabishara wazawa kumiliki viwanda kwa maaendeleo ya nchi.

''Tumekuwa na mambo mengi lakini dhamira ya Serikali kwa miaka mitano inayokuja ni kujenga viwanda na kuwezesha wafanyabishara wazawa kuvimiliki,''alisema. 

Maonesho hayo ni ya nne tangu kuanza kuonyeshwa nchini ambayo yanaendelea kwa siku tatu katika viwanja vya Daimond Jubilee jijini Dar es Salaam.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com

No comments: