Thursday, September 03, 2015

MAGUFULI AFUNGA KAZI MKOANI MTWARA,AHIDI KUSHUSHA BEI YA VIFAA VYA UJENZI

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli,akiwahutubia wananchi wa mji wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza kwenye mkutano wa kampeni jana jioni katika uwanja wa Mashujaa. 

Dkt John Magufuli amesema kuwa iwapo atachaguliwa kuwa Rais katika uchaguzi mkuu mwaka huu ,Serikali yake itashusha bei ya vifaa vya ujenzi hasa bati na saruji,amesema kuwa serikali yake inataka kurahisisha maisha ya watanzania wote na hivyo atapunguza bei ya saruji na bati na hilo litafanikiwa kwa kupunguza ushuru wa vifaa hivyo. 

"Serikali ya Magufuli nataka iwe ya kurahisisha maisha ya wananchi wake.Moja ya mambo ambayo ninedhamiria kuyafanya ni kupunguza bei ya bati na saruji.Nataka kuona watu wanajenga nyumba nzuri na za kisasa, hivyo lazima tushushe bei ya vifaa vya ujenzi,alisema Dk.Magufuli.

Alisema anatambua kiu ya watanzania ni kutaka mabadiliko ya maendeleo na kwamba Serikali yake itasimamia kuleta maendeleo ya wananchi na kazi hiyo anaiweza na ndio maana anaomba urais. " Ndugu zangu watanzania serikali ya Magufuli inakuja kuendelea pale ambapo awamu nyingine zimeishia.Tumetoka mbali ,tupo mbali na tunakwenda mbali.Nataka tuwe na maendeleo makubwa na hilo serikali yangu ndio kazi itakayofanya,"alisema Dk.Magufuli huku wananchu wakimshangilia kwa mayowe.

Dk Magufuli tayari hadi sasa amefanya mikutano ya kampeni katika mikoa 6 ya Katavi, Rukwa, Mbeya, Njombe, Ruvuma na Mtwara. ambapo akishinda uchaguzi ameahidi mambo mbalimbali kama vile Eimu ya bure kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne, kujenga reli kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay mkoani Ruvuma, kushusha bei ya vifaa vya ujenzi na kutoa sh. mil. 50 kwa kila kijiji za kuwakopesha wanawake na vijana kuendeleza miradi na biashara zao kwa lengo la kuwaletea maendeleo

  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli,akiwahutubia wananchi wa mji wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza kwenye mkutano wa kampeni jana jioni katika uwanja wa Mashujaa. 

Dk Magufuli tayari hadi sasa amefanya mikutano ya kampeni katika mikoa 6 ya Katavi, Rukwa, Mbeya, Njombe, Ruvuma na Mtwara. ambapo aakishinda uchaguzi ameahidi mambo mbalimbali kama vile ile ya bure kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne, kujenga reli kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay mkoani Ruvuma, kushusha bei ya vifaa vya ujenzi na kutoa sh. mil. 50 kwa kila kijiji za kuwakopesha wanawake na vijana kuendeleza miradi na biashara zao kwa lengo la kuwaletea maendeleo 
Wakazi wa mji wa Mtwara wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM,unaofanyika jioni ya jana kwenye uwanja wa CCM,wakimsikiliza mgombea Urais wa chama hicho Dkt John Pombe Magufuli.

 Dk Magufuli akizungumza na mtoto Riziki Faraji na pia alimpa kiasi kadhaa  cha fedha kwa ajili ya kununulia sare ya shule alipomuona wakati msafara wake ulipozuiwa na wananchi katika Kijiji cha Kitama A, mkoani Mtwara


  Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kata ya Ziwani Mtwara Vijijini

 Mgombea Ubunge wa jimbo la Mtwara mjini,Murji Hasnein Mohamed akiwasalimia maelfu ya wananchi wa mji wa Mtwara waliofurika kwenye uwanja wa Mashujaa katika mkutano wa kampeni za CCM,jioni ya jana ambapo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli aliwahutubia wananchi hao .
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akijiachia jukwaani pamoja na wasanii wa kundi la Yamoto Band kwenye uwanja wa Mashujaa mkoani Mtwara,ambapo Dkt Magufuli aliwahutubia wananchi hao waliofurika kwa wingi.
  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akijiachia jukwaani pamoja na wasanii wa kundi la Yamoto Band kwenye uwanja wa Mashujaa mkoani Mtwara,ambapo Dkt Magufuli aliwahutubia wananchi hao waliofurika kwa wingi.

No comments: