Monday, September 14, 2015

DR. JOHN POMBE MAGUFULI:NITAUNDA BARAZA LA MAWAZIRI WAADILIFU, WAKWELI NA WACHAPAKAZI

1
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini Igunga jana ukihudhuriwa na maelfu ya wananchi waliokuja kumsikiliza mgombea huyo wakati akiwaomba kumpigia kura za ndiyo katika uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani ifikapo Oktoba 25 mwaka huu nchini kote.
Dr. John Pombe Magufuli akizungumza katika mkutano huo amesema mara atakaposhinda uchaguzi huo na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ataunda baraza la mawaziri walio waadilifu, Wachapakazi , Wakweli na wenye moyo thabiti wa kuwatumikia watanzania ili kuwaletea maendeleo wananchi na kukuza uchumi wa taifa,  Hasa katika suala zima la kujenga Viwanda vya bidhaa mbalimbali hasa vya Nguo na viatu vya ngozi, mikoba ya ngozi na mikanda kutokana na wingi wamifugo iliyopo nchini.
2
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Igunga katika mkutano wake wa kampeni jana.
3
Wananchi wa Igunga wakinyanyu  mikono yao juu huku wakiimba wimbo wa kisukuma Alinselema wakati Dr. Magufuli akihutubia mkutano huo.
45
Mmoja wa vijana akiwa ameshikilia bango lenya maandishi ya Magufuli ni Obama wa Tanzania yakimsifu mgombea huyo  Dr. John Pombe Magufuli.
6
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akimkabidhi ilani ya uchaguzi mgombea ubunge wa jimbo la Manonga mkoani Tabora Bw. Seif Said Gulamali.
7
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akionyesha ilani ya uchaguzi kabla ya kumkabidhi mgombea ubunge wa jimbo la Igunga Dr. Dalali Peter Kafumu mjini Igunga.
9
Baadhi ya vijana wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akihutubia mjini Igunga.
10
Viongozi mbalimbali wakiwa wamekaa meza kuu wakati mkutano ukiendelea mjini Igunga.
11
Mawasiliano yakiendelea lakini bila kumsahau Dr. John Pombe Magufuli kama inavyoonekana katika picha.
12
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akipanda jukwaani kuzungumza na wananchi na kuwaomba kura mjini Igunga jana.
14
Kada wa CCM na Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu nchini Bw. Amon Mpanju akimpigia debe Dr John Pombe Magufuli.
15
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wakati alipowasili mjini Igunga  kwa ajili ya Mkutano wa Kampeni.
16
Msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli ukiwasili katika eneo la mkutano mjini Igunga,
17
Hapa kila mtu ni Magufuli tu mikononi mwao
18
Kijana huyu anasema CCM Mbele kwa mbele “Hapa Kazi Tu” na Msumeno wake.
19
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Kishapu Mh Suleiman Nchambis.
20
Wananchi wa Kishapu wakishangilia wakati Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia.
21
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi mjini Kishapu huku vijana wakiwa wamepanda juu ya miti wakimsikiliza.
22
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Kishapu
24
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akizungumza na mgombea ubunge wa jimbo la Kishapu Mh Suleiman Nchambis wakati alipowasili mjini Kishapu.
26
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Maganzo akielekea mjini Kishapu. 
27
Mama huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja akifurahia hotuba ya Dr. John Pombe Magufuli katika mji wa Maganzo.
29
Baadhi ya madiwani wa Maswa wakiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Maswa. 
30
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi mara baada ya kuhutubia mkutano wake wa kampeni mjini Igunga jioni ya jana.
31
Wananchi wakiondoka mkutanoni mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kampeni wa Dr. John Pombe Magufuli mjini Igunga.
32
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwasalimia watawa  wakati alipokuwa akiodoka baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni  mjini Igunga
33
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa Igunga mara baada ya kuhutubia mkutano wake wa kampeni jana jioni mjini humo.
Post a Comment