Monday, January 26, 2015

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA NHIF YATOA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI WASIO KATIKA SEKTA RASMI

 001
Meneja Kiongozi wa Bima ya Afya CHIF Kanda ya Ilala, Christopher Mapunda akifunga semina ya siku tatu ya viongozi wa SACCOS za wajasiriamali zilipo Mansipaa ya Ilala iliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWEBLOG
002
Afisa Matekelezo Bima ya afya NHIF kanda ya Ilala, Hipoliti Lello akifafanua jambo kuhusina na kiwango cha uchangiaji kwa wajasiriamali ni shilingi za kitanzania 76,800 ambacho kinamwezesha mjasiriamali kuweza kupata matibabu kwenye zahanati, kituo cha afya, hospital za wilaya, mikoa na za rufaa nchini.
003
Mjumbe wa Bodi Saccos ya wajasiriamali, Bw, Adela Raymond akichangia mada yake wakati wa semina hiyo
004
Viongozi wa Bima ya afya NHIF pamoja na wajasiriamali wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo.
…………………………………………………………………………………………………
BIMA YA AFYA nchini (NHIF) imetoa mafunzo ya umuhimu wa Bima ya afya kwa wajasiriamali wasiyokuwa katika sekta rasmi lenye lengo la kuhamasisha jamii kwenye makundi mbalimbali kujiunga na mfuko huo.
Akifunga semina ya siku tatu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki,Meneja Kiongozi wa Bima ya Afya Kanda ya Ilala, Christopher Mapunda alisema kwamba bima ya afya nchini itaendelea kutoa mafunzo kwa wanajamii ili waweze kujiunga na mfuko wa bima ya afya nchini.
“Mfuko wa bima ya afya nchini utaendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali hasa yale yaliyopo kwenye sekta isiyo rasmi nchini kuweza kuweka akiba kwa ajili ya bima ya afya kwa manufaa yao na vizazi vyao,” alisema Bw, Mapunda
Bw Mapunda aliongeza kwamba mafunzo hayo ya siku tatu yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa baada ya washiriki kujitokeza kwa wingi na kuonyesha nia ya kujiunga na mfuko huo kwa maisha ya baadaye.
Aliongeza kwamba dhamira na dira ya mfuko huo ni kuwahikisha watanzania wengi wanajiunga na mfuko sambamba na kupata elimu kuhusu bima ya afya kwa maisha yao.
Alisema kwamba mfuko huo utaendelea kutoa mafunzo juu ya umuhimu wa bima ya afya na wana mpango wa kuendelea na mafunzo mpaka visiwani na si bara. 
Kwa upande Hipoliti Lelo, Afisa Matekelezo Bima ya afya kanda ya Ilala alisema kwamba wameamua kuleta bima hiyo afya kwa wajasiriamali wasio katika sekta rasmi ili waweze kupata uhakika wa matibabu kupitia mfuko wa bima ya afya nchini
Alisema kwamba kiwango cha uchangiaji kwa wajasiriamali ni shilingi za kitanzania 76,800 ambacho kinamwezesha mjasiriamali kuweza kupata matibabu kwenye zahanati, kituo cha afya, hospital za wilaya, mikoa na za rufaa nchini.
Alifafafua kwamba hiyo ni fursa pekee kwa mjasiriamali nchini kuweza kupata matibabu hata kama hayupo kwenye mfumo rasmi wa ajira nchini.
Naye Mjumbe wa Bodi Saccos ya wajasiriamali, Bw, Adela Raymond alisema kwamba waliona umuhimu wa kujiunga na mafunzo kwanza ya bima ya afya kutokana na matatizo yaliyokuwa yanajitokeza kwa wanachama wao hasa wakati wa marejesho.
“Mwanachama wetu wa Saccos akiumwa tu anakwambia hawezi kuleta marejesho na fedha hizo ametumia kwa ajili ya matibabu kwa hiyo tukaona kuna umuhimu wa chama kuijunga na mfuko wa bima ya afya nchini ,” alisema 
Alifafanua kwamba umuhimu wa bima hiyo kwa wanachama ni kwamba wanaweza kurudisha marejesho na kuendelea kupata matibabu kupitia mfuko huo wa bima nchini.

No comments: