TIMU YA WATAALAMU KUTOKA WIZARA YA UCHUKUZI WATEMBELEA OFISI ZA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA(TCAA)
Meneja wa Kitengo cha taarifa za Usalama wa Usafiri wa Anga, Bw. Deodore Mushi akitoa maelezo ya namna ya mashine mbalimbali zinazotumika katika chumba maalum cha kutolea taarifa za usafiri wa Anga zinavyofanya kazi, kwa wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, waliotembelea katika ofisi hizo jana asubuhi kufanya tathimini ya utoaji wa huduma katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA). Wa Kwanza kulia ni Afisa Usafirishaji kutoka Wizara ya Uchukuzi, Bw. Biseko Chiganga (aliyevaa koti jeusi), wa pili kushoto kwa Chiganga ni Afisa Usafirishaji, Bw Benjamin Mbimbi na tatu kutoka kushoto ni Afisa Usafirishaji, Bw. Said Marusu.
Meneja wa Kitengo cha Uongozaji Ndege, Mwanajuma Kombo, akifafanua jambo kwa wataalamu kutoka Wizara ya Uchukuzi, waliotembelea kituo cha kuongozea ndege jana asubuhi kufanya tathmini ya utoaji wa huduma katika usafiri wa Anga katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA).
No comments:
Post a Comment