Kamishna mpya wa Ardhi nchini Dk Moses Kusiluka ambaye pia ni mtaalamu aliyebobea masuala ya Real Estate Finance and Investment akitoa somo kwenye kongamano la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, Arusha, Amepongeza uwekezaji unaofanywa na NHC na akazungumzia kwa kina kuhusiana na masuala muhimu ya kuzingatia katika uendelezaji miliki na pia maamuzi muhimu ya kifedha kuyafanya ili kuweza kuwa na ufanisi katika sekta ya uendelezaji miliki. Kongamano linakusudia kuwajengea uwezo wa kiuongozi wa kusimamia uuzaji wa nyumba zinazojengwa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini. Katika kongamano hilo, mada mbalimbali zinaendelea kutolewa ikiwemo kuwajali wateja, misingi ya uhusiano na ujenzi wa taswira ya Shirika na uwekezaji katika sekta ya usimamizi na uendelezaji wa Miliki.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi akiwakaribisha watoa maada mbalimbali kwenye kongamano hilo.
Mtaalamu Mshauri wa masuala ya Menejimenti wa Chuo Kikuu cha Uongozi Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI), Peter Kalunda Kiuluku akitoa mada kwenye kongamano la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, Arusha.Mtaalamu Mshauri wa masuala ya Biashara wa Chuo Kikuu cha Uongozi Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI), Christine Magunje akitoa mada kwenye kongamano la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, Arusha.
Washiriki mbalimbali wakifuatilia kwa makini kongamano hilo linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, linafanyika kwa wiki nzima.
Washiriki mbalimbali wakifuatilia kwa makini kongamano hilo linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, linafanyika kwa wiki nzima.
Washiriki mbalimbali wakifuatilia kwa makini kongamano hilo linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, linafanyika kwa wiki nzima
Comments