Monday, January 19, 2015

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AMALIZA ZIARA YAKE MKOA WA MAGHARIBI

1Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia mti wa viungo aina ya Mdalasini wakati akipata maelezo kutoka kwa Othman Mohamed  mwenyekiti wa kikundi Kinachoendesha shamba la Spice Solution Farm lililopo Mwakaje  jimbo la Mfenesini Zanzibar  wakati aliposhiriki pia shughuli za upandaji wa miti katika shamba hilo, Katika ziara hiyo ambayo ni ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2010 Kinana Anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MFENESINI -ZANZIBAR)2Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kupanda miti katika shamba la Spice Solution Farm Mwakaje Mfenesini.3Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia pilipili zilizolimwa katika shamba hilo huku akipata maelezo. 6Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia viongo mbalimbali vilivyosagwa na kusindikwa tayari kwa kuuza kwa wateja.7Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kufukia mabomba katika mradi wa maji wa Mbuzini jimbo la Mfenesini huku akishirikiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi Ndugu Yusuf Mohamed Yusuf.8Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Mama Khadija Issa Kibwana mara baada ya kuzindua mradi wa maji Mbuzini jimbo la Mfenesini.5Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na kikundi cha akina mama wajasiriamali cha Mshikamano Daima Kilichopo Mtopepo jimbo la Mtoni mjini Zanzibar.10Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto na Waziri Kiongozi Mstaafu Mh. ShamsiVuai Nahodha  wakishiriki katika ujenzi wa ofisi ya CCM tawi la Bububu.11Waziri Kiongozi Mstaafu Mh. Shamsi Vuai Nahodha  kushoto akiteta jambo na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM wakati wa mkutano wa ndani uliofanyika kwenye ofisi ya CCM tawi la Bububu.12Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa Halimashauri kuu ya  wilaya ya Mfenesini.13Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Ndugu Yusuf Mohamed Yusuf akizungumza katika mkutano huo wa ndani.14Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Kikwajuni Mh. Masauni Yusuf Masauni.15Baadhi ya wajumbe wakiwa katika mkutano wa ndani17Balozi Ali Karume akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Geji jimbo la Mtoni mjini Zanzibar.19Baadhi ya wananchi na wana CCM wakiwa katika mkutano huo.20Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Geji Mtoni mjini Zanzibar.21Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Vuai Ali Vuai akizungumza na wananchi katika mkutano huo amewataka wazanzibari kupiga kura ya ndiyo ifikapo aprili 30 mwaka huu ili kuipitisha katiba mpya iliyopendekezwa.22Baadhi ya wanaCCM wakinyoosha mikono yao juu kukubali kupiga kura ya ndiyo katiba mpya iliyopendekezwa ifikapo Aprili 30 mwaka huu.23Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika mkutano huo.

No comments: