WATANZANIA WATAKIWA KUITUMIA VYEMA FURSA YA KIMATAIFAKATIKA MAONYESHO YA BIASHARA

unnamed (1)Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akitoa nasaha zake kwa Washiriki wa Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman, kushoto kwake ni Naibu Balozi wake Bw.Juma Othman.
unnamed (3)Baadhi ya Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini humo Bw. Ali Ahmed Saleh alipokuwa akiwanasihi Washiriki hao.
unnamed (4)Baadhi ya Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini humo Bw. Ali Ahmed Saleh alipokuwa akiwanasihi Washiriki hao.
unnamed (5)8 Mkuu wa Msafara wa Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika mjini Mascut, nchini Oman Bi Khadija Batashy akitoa shukran zake kwa niaba ya wenzake baada ya kupewa nasaha na Balozi wa Tanzania nchini humo Bw. Ali Ahmed Saleh wa katikati, kulia kwake ni Naibu Balozi Bw.Juma Othmanunnamed (7)Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akiwa katika picha ya Pamoja na Wakuu wa Msafara wa Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman kulia ni Masha Hussein na kushoto ni Khadija Batashy. Picha na Faki Mjaka.
unnamed (8)Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akiwa katika picha ya Pamoja na Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman mara baada ya kuwapa nasaha zake. Picha zote na Faki Mjaka.
unnamed (9)Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akisalimiana na Mwandishi wa Chanel Ten Said Makala Ofisini kwake alipowaita kwa lengo la kuwapa nasaha Washiriki wa Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman. Picha na Faki Mjaka.unnamed (82)2 Mkuu wa Utawala Ubalozi wa Tanzania nchini Oman Abdallah Kilima kushoto akimkaribisha  Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh kulia kutoa nasaha zake kwa Washiriki wa Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman. Katikati ni Mkuu wa Msafara wa Watanzania hao Bi Khadija Batashy.
………………………………………………………………
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar, akiwa Mascut-Oman 22/01/2015
Watanzania wanaoshiriki katika Maonesho Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea nchini Oman wametakiwa kuitumia vyema fursa ya kimataifa walioipata kwa kufuata vyema Miongozo waliyopewa ili ziara yao iweze kuleta Tija.
Miongozo hiyo ni pamoja na Mashirikiano miongoni mwao,kujituma kwa bidii na kutumia lugha nzuri katika Maonesho hayo kwa kuzingatia kuwa Wananchi wengi wa Omani wanaelewa vyema Lugha ya Kiswahili.
Wito huo umetolewa na Balozi wa Tanzania nchini Oman Mh. Ali Ahmed Saleh wakati alipokuwa akitoa nasaha zake kwa Washiriki wa Maonesho hayo Ofisini kwake Mascut nchini Oman.
Amesema Tanzania ni nchi inayoongoza kuwa na Mahusino mema na Oman hivyo Washiriki hao wanapaswa wafanye kazi zao kwa bidii na kuzingatia kanuni na Maadili ya Oman.
Balozi Saleh ameongeza kuwa kufuata kanuni na sheria za Oman kutawafanya Wajasiriamali hao wa Tanzania kufanyakazi zao kwa utulivu bila ya kupata usumbufu jambo ambalo litazidi kuimarisha mahusiano mema kati ya Tanzania na Oman.
Amebainisha kuwa Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete aliyoifanya mwaka jana nchini humo imezidi kuyaweka pazuri mahusiano na kwamba Washiriki hao wanapaswa wayatunze na kuyalinda.
“Ndugu zangu Tanzania ina nafasi ya kipekee nchi Oman,tunaheshimiwa sana kuliko nchi yoyote hasa baada ya ziara ya Rais Kikwete, naomba Mahusiano haya muyaendeleze kwa kufanya kazi zenu kwa bidii na kuchunga maneno yenu maana hawa Waoman wanakijua vyema Kiswahili Mkiwasema Wanafahamu” Alinasihi Balozi Saleh.
Ameongeza kuwa Raia wa Oman wanautamaduni wa Kumsifu na Kumtukuza Mfalme wao Sultan Qabus kwa mengi mazuri aliyowafanyia hivyo Watanzania hao wanapaswa kulifahamu hilo na kulichukulia Tahadhari.
Balozi Saleh amesema Mashirikiano miongoni mwao ni Jambo muhimu na kwamba wote wamekuja kwa Niaba ya Jamhuri ya Tanzania na Sio Bara au Visiwani.
“Kitu kingine Mufahamu kuwa hapa Tunaiwakilisha Tanzania kwa hiyo Uzanzibari na Ubara usiwepo maana mukiupa nafasi utamusumbua,Tusimameni katika Jina moja tu la Utanzania ambalo ndio uwakilishi wetu kimataifa” Alisema Balozi.
Aidha ametoa Wito kwa Wajasiriamali ambao hawakupata fursa ya kushiriki Maonesho hayo kutokata tama na kuamini kuwa ipo siku nao watapata nafasi ya kushiriki Maonesho ya kimataifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Msafara wa Watanzania Wanaoshiriki Maonesho hayo Bi Khadija Batashy alimshukuru Balozi Saleh na Wasaidizi wake kwa Mapokezi mazuri na Nasaha alizozitoa.
Aidha Bi Khadija alimuahidi Balozi huyo kuzifanyia kazi nasaha hizo ikiwemo kujituma, kuzidisha mashirikiano na kutumia lugha nzuri ili kuwavutia wateja katika Maonesho hayo.
Awali Mkuu wa Utawala katika Ofisi ya Ubalozi Bw. Abdallah Kilima wakati akimkaribisha Balozi aliishukuru nchi ya Mascut kwa kuzidi kuongeza njanja za kuimarisha mashirikiano ikiwa ni pamoja na Mwaliko wa Maonesho hayo.
Kilima aliwataka Washiriki hao kuwa kitu kimoja na kusaidiana kwa hali na mali jambo ambalo litaipatia sifa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Maonesho hayo ya muda wa mwezi mmoja ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, huanza kila ifikapo saa 10 za jioni na kufungwa saa 04 usiku kwa majira ya nchi ya Omani ambapo Washiriki huonesha bidhaa za nchi zao na Watu kunua bidhaa hizo.

Comments