WAJUMBE WA BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA WATAKIWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUTEKELEZA WAJIBU WAO KWA KUJITOLEA ZAIDI.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) mara baada ya kuzindua Balaza la 13 la Michezo leo jijini Dar es Salaam.Waliokaa kutoka kushoto ni Katibu wa Baraza la Michezo Zanzibar, Naibu Kaibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel, Mwenyekiti wa BMT Bw. Dioniz Malinzi na mjumbe wa BMT Mhe. Zainab Vulu (MB).
Picha zote na Frank Shija, WHVUM.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akitoa nasaha kwa wajumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wakati akizindua Balaza la 13 la Michezo jana jijini Dar es Salaam.Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel na wa mwisho kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo. Wajumbe waliohudhuria hafla hizo ni pamoja na ,Mkurugenzi wa PSPF Adam Mayingu, Zacharia Hans Pope, Jamal Rwambow, Mkurugenzi wa Operesheni wa NSSF Crescentius Magori ,wajumbe wengine ni Alex Mgongolwa, Jennifer Mmasi Shang’a, Mhe. Zainabu Vulu (MB), Mohamed Bawaziri na Mwl. Zaynab Mbiro.Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Dioniz Malinzi akitoa neno lashukrani mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Baraza la 13 la Michezo jana jijini Dar es Salam. Pembeni ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel na wa mwisho kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo.
Baadhi ya wajumbe wa Barala la Michezo la Taifa (BMT) wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri wakati wa hafla ya uzinduzi wa baraza hilo (jana) jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Zacharia Hanspope, Crescentius Magori ambaye, Adam Mayingu ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Mohamed Bawaziri na Mwl. Zaynab Mbiro
Comments