KAMPUNI YA UWEKEZAJI YA UTT YAHIMIZA USHIRIKIANO WA SOKO LA HISA KWA NCHI ZA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI
Ofisa Mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni ya Uwekezaji
ya UTT, Migangala Simon.
Ofisa Mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT, Migangala Simon (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu ushirikiano wa uwekezaji katika soko la hisa kwa nchi zinazounda jumuia ya Afrika Mashariki.
Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Uwekezaji ya UTT imesema ushirikiano wa uwekezaji katika soko la hisa wa nchi za jumiya ya Afrika Mashariki utaleta tija kwa nchi hizo.
Akizungumza Dar es Salaam leo Ofisa Mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni hiyo, Migangala Simon alisema uwepo wa ushirikiano utasaidia hata nchi moja ikiwa na matatizo iwe rahisi kusaidiana.
“Kwa mfano Tanzania sasa hivi inaelekea katika uchaguzi mkuu ambao unatarajia kufanyika Oktoba mwka huu inavyoelekea hivyo fedha nyingi zitatumika lakini kukiwepo na ushirikiano na umoja ni lazima nchi nyingine kusaidia kupitia soko la hisa,”alisema.
Alisema kampuni hiyo ina jumla ya mifuko mitano,kuna mfuko wa umoja,wekeza maisha, mfuko wa watoto,mfuko wa ukwasi na mfuko wa jikimu.
Simon alisema mifuko yote ina lengo la kusaidia wananchi wote walio katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
“Pia huwa tunawasaidia watoto katika maendeleo yao hapa nchini hususani elimu watoto hao ni wale walio chini miaka 18,”alisema.
Simon alitumia fursa hiyo kuwaomba watanzania kujiunga na kampuni hiyo na kuweka hisa zao ambapo watapata gawio kubwa kulingana na hisa walizoweka. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com
Comments