Ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Mikoani

 Mkurugenzi wa Mikoa na Utawala wa NHC Bw. Raymond Mndolwa (aliyenyosha mkono juu) akiekeza jambo wakati alipokuwa kwenye ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC kwenye mradi wa nyumba za Makazi Wilayani Monduli jana.
 Mkugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akikagua nyumba za makazi za kuuza  zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akipewa maelezo ya mradi wa nyumba za kuuza za makazi zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli na Msimamizi wa mradi huo Bw. Hassan Bendera.
Hii ni sehemu ya nyumba za makazi zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli kama sehemu ya juhudi za Shirika hilo za kuwezesha wananchi wengi kumiliki nyumba. Nyumba hizi zinajengwa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini.
Msimamizi wa mradi wa nyumba za makazi zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli Bw. Hassan Bendera (mwenye koti jekundu kushoto) akitoa maelezo  kwa ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC,Twalib Mbasha  yanayohusu  hatua za utekelezaji wa mradi wa nyumba za makazi zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli.
 Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akikagua mchoro wa ujenzi wa nyumba za makazi zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli.
 Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Twalib Mbasha na kuhimiza Halmashauri hiyo kukamilisha ulipiaji wa nyumba hizo ili Shirika liongeze kasi ya kukamilisha mradi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Twalib Mbasha na kuhimiza Halmashauri hiyo kukamilisha ulipiaji wa nyumba hizo ili Shirika liongeze kasi ya kukamilisha mradi huo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli (katikati), Twalib Mbasha akiuonyesha ujumbe wa NHC eneo lililotengwa kwa ajili ya kujenga nyumba ambalo alisema lina miundombinu yote muhimu ikiwemo umeme na maji

Comments