Tuesday, January 20, 2015

ZAIDI YA BILIONI 29 ZINAWASUBIRI WATEJA WA VODACOM KUPITIA PROMOSHENI YA JAYMILLIONS


Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (kualia) akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kuchezesha droo ya sita ya promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na kampuni hiyo iliyofanyika leo,ambapo jumla ya wateja 947 wamejishindia muda wa maongezi na wateja watano wamejishindia shilingi Milioni 1/- kila mmoja kutoka kushoto ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha,Mrisho Millao na Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo Mathew Kampambe.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika droo ya droo ya sita ya promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na kampuni hiyo iliyofanyika leo, ambapo jumla ya wateja 947 wamejishindia muda wa maongezi na wateja watano wamejishindia shilingi Milioni 1/- kila mmoja.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

Wateja wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania wametakiwa kuchangamkia promosheni ya Jaymillions kwa kutuma ujumbe wenye neno JAY kwenye namba 15544 ili kujua kama iwapo namba zao zimeibuka na ushindi katika droo inayofanyika kila siku.

Akiongea baada ya kumalizika kwa droo ya sita ya promosheni hiyo ambayo ilifanyikiwa kupata washindi wa muda wa maongezi kufikia idadi ya 947 na kutokufanikiwa kupata mshindi wa fedha taslimu na kubakia na idadi ileile ya washindi watano waliojishindia shilingi Milioni moja moja kila mmoja,Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amesema kuwa kila mteja wa Vodacom anashirikishwa katika promosheni hii na anachotakiwa kufanya kutuma ujumbe wa kujua kama ameibuka kuwa mshindi wa siku.

“Mfumo wa promosheni hii kila namba ya mteja wa Vodacom inashirikishwa kinachotakiwa ni kutuma ujumbe yaani kucheki kujua kama wameshinda ili wasipoteze bahati zao, mpaka sasa kuna wateja watano wamejishindia shilingi milioni moja kila mmoja na wengine 947 wamejishindia muda wa maongezi”.Alisema.

Nkurlu aliongeza kusema kuwa bado kuna Shilingi Bilioni 29,995,000,000/= za promosheni hii inayoendelea ya Jaymillions zikiwasubiria wateja wa Vodacom na watanzania kwa ujumla wanaoshiriki katika promosheni hii. Promosheni hii itafanyika kwa siku 100 mfululizo na Vodacom  imepanga kutoa mshindi mmoja wa Sh. 100m/-, washindi kumi wa Sh. 10m/- na washindi thelathini wa Sh. 1m/- KILA SIKU kwa siku mia moja! Pia washindi elfu kumi watapokea muda wa maongezi wa bure wenye thamani ya Sh. 1000/-
Alimalizia kwa kusema kuwa mara tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi utakaomjulisha kama ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo atajulishwa hivyo na kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata. “Kila SMS inagharimu Sh. 300/- tu”.Alisema

No comments: