Friday, January 16, 2015

WAZIRI FENELLA AZINDUA UUZAJI WA FILAMU ZA KITANZANIA KWA NJIA YA MTANDAO

unnamedWaziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukungara(MB) akiteta jambo na msani wa filamu nchini Bi. Lulu Michael wakati wa hafla ya kuzindua mfumo wa uuzaji wa Filamu nchini kupitia mtandao ulioanzishwa na Kampuni a Usambazaji wa Filamu Proin Poromotion jana jijini Dar es Salaam.Picha na Frank Shija,WHVUM
unnamed1Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukungara(MB) akizungumza na wadau wa tasnia ya filamu (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kuzindua mfumo wa uuzaji wa Filamu nchini kupitia mtandao ulioanzishwa na Kampuni a Usambazaji wa Filamu Proin Poromotion jana jijini Dar es Salaam.
unnamed2Mwenyekiti wa Kampuni ya Proin Promotion Bw. Johnson Lukaza akizungumza na wadau wa tasnia ya filamu (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kuzindua mfumo wa uuzaji wa Filamu kupitia mtandao jana jijini Dar es Salaam.unnamed3Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukungara(MB) akibofya kitufe cha Kompyuta mpakato (laptop) kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma ya kununua filamu mtandaoni jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo na kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Proin Promotion Bw. Johnson Lukaza.unnamed6Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akifuatilia filamu ya Neema ya Mungu iliyozinduliwa wakati wahafla ya uzinduzi wa mfumo wa kununua filamu mtandaoni ulionzishwa na Kampuni ya Proin Promotion jana jijini Dar es Salaam aliyevaa suti katikati ni Rais wa Shirikisho la Wasanii wa Filamu Tanzania (TAFF) Bw. Simon Mwakifamba.

No comments:

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKITUNUKIWA NISHANI YA HESHIMA YA JUU YA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI (THE GRAND CORDON)

Dar es Salaam, 14 Agosti 2025  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Nish...