Wednesday, January 21, 2015

MKOA WA ARUSHA WATOA KIWANJA KWA AJILI YA UJENZI WA CHUO KIKUU HURIA

Mkuu wa mkoa wa Arusha Daud indexNtibenda ameamua kutoa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu huria cha Arusha baada ya kutoridhishwa na majngo ya chuo hicho na kudai kuwa hayana hadhi ya chuo hicho na kuwa yanaonekana kama nyumba ya mtumishi wa serikali kuishi.
Pia mkuu huyo ametoa siku 30 kwa Afisa Ardhi wa mkoa huo kutafuata kiwanja kwa ajili ya kuanza ujenzi rasmi wa chuo ambacho kitakuwa na hadhi ya kuitwa chuo Kikuu.
Aliyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kukitembelea na kuonana na wafanyakazi na kufanya nao maongezi pamoja na wahitimu wa chuo hicho kwenye mahafali ya 26 chuo hapa jijini hapa.
Ntibenda alisema kuwa majengo hayo ya chuo yamemsikitisha kiasi cha kutoa machozi hali ambayo inatakiwa kupatiwa ufumbuzi ndani ya mwezi mmoja ilikuongeza umaridadi wa elimu inayotolewa chuoni hapo.
“Kweli kabisa mimi kama mkuu wa mkoa ambaye raisi ameniona nafaa kuongoza mkoa huu sintakubali kuona eti wanafunzi hata kama ni wa vyuo huria wanasoma katika majengo kama haya badala yake nitahakikisha kuwa wanahama hapa na mnapata majengo mazuri na ni haki yenu ninyi wanafunzi”aliongeza Ntibenda
Alifafanua kuwa chuo hicho hasa masomo huria kinapokuwa na majengo mazuri kinasaidia wanafunzi kuweza kupata hamasa kubwa katika masomo lakini kinapokuwa na majengo ambayo hayana hadhi ya chuo basi hayapendezi wala kuvutia katika mazingira ya masomo.
“Pamoja na kuwa mmesoma na matokeo yenu ni mazuri sana tena ya kupigiwa mfano mimi nasema bado kunauwezekano wa kufanya chuo hichi kikawa bora ni kwamba sote sisi tukiungana na tuwe kimoja”aliongeza Ntibenda
Katika hatua Nyingine katibu wa chama cha wanafunzi wa chuo kikuu huria Kasimu Mfinanga alisema kuwa mapendekezo ya chuo hicho ni pamoja na kusogeza huduma ya elimu karibu zaidi na wananchi hasa wale wa vijini lakini hata kwenye Wilaya Zote.
Mfinanga alimaliza kwa kusema kuwa mapendekezo mengine ni pamoja na kuendelea kuelimisha jamii umuhimu wa kujiunga nacho kwani amendeleo thabiti hayapatikani bila ya kuwa na elimu.

No comments: