Picha zote na Hussein Makame, MAELEZO
…………………………………………………………………………………..
Hussein Makame, MAELEO, Pwani
KAMATI ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imeeleza kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya maji ya Kibiti na Ikwiriri iliyopo wilayani Rufiji mkoani Pwani kutokana na kuonesha mafanikio makubwa.
Hayo yamesemwa na Kiongozi wa Wajumbe wa Kamati hiyo Amina Makilagi (Mb) baada ya kukagua miradi hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maji Tanzania Bara inayofanywa na baadhi ya wajumbe wa kamati katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.
Alisema pamoja na miradi hiyo kukabiliwa na changamoto mbalimbali, imeweza kutoa huduma kwa wakazi 34,428 wa maeneo hayo na wananchi kupitia viongozi wao kuthibitisha mafanikio ya miradi hiyo.
“Kimsingi tumefurahishwa na maendeleo ya utekelezaji wa miradi hii,tulipokuwa Dar es Salaam tuliambiwa miradi ya Kibiti na Ikwiriri imekamilika na inaendelea vizuri na wananchi wamekiri hilo kupitia kwa viongozi wao” alisema Makilagi.
Mradi wa Kibiti wenye visiwa virefu vitano vinavyozalisha maji safi na salam, huzalisha meta za ujazo 55 kwa saa huku ule wa Ikwiriri ukiwa na kisima kirefu chenye urefu wa meta 60 na kipenyo cha 14 cha ujazo na wenye una matanki mawili yenye uwezo wa mita za ujazo 500 kila moja.
Mtandao wa mradi huo wa maji una pampu inayoweza kusukuma maji kwa saa 12 na bomba kuu lenye urefu wa kilometa 10 na mabomba yanayosambaza huduma hiyo kilometa 21 na vituo vya kuchotea maji 5.
Hata hivyo, Makilagi aliwataka wakazi wa maeneo husika kuacha tabia ya kuiba vipuri vya mabomba ya miradi hiyo kwani Serikali imewapelekea huduma hiyo kuondokana na ukosefu wa huduma ya maji safi na salama.
Alisema kamati hiyo imekagua miradi hiyo kutekeleza jukumu la bunge la kuisimamia serikali katika shughuli za maendeleo ambapo hatua hiyo italifanya bunge kujihakikishia kile kinachotekelezwa na serikali katika miradi hiyo.
Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Maji wa Kibiti Mhandisi Juma Ndaro alieleza changamoto zinazokabili mradi huo ikiwemo kutokuwepo kwa mamlaka ya kudumu ya maji kwa kuwa mji mdogo wa Kibiti bado haujatangazwa rasmi kuwa Mji mdogo.
Changamoto nyingine inayokwaza mradi huo ukatikaji wa umeme unaosababisha mota za maji kuungua na changamoto hiyo kusababisha upatikanaji wa maji kutokuwa wa kudumu kutokana na kutegemea umeme.
Katika mradi wa Ikwiriri, Mjumbe wa Bodi ya Maji ya Ikwiriri Kasimu Mpeliwe ambaye ni mwakilishi watumiaji wa maji Ikwiriri, aliishukuru Serikali kuwapelekea mradi huo kwani umeonesha mafanikio makubwa.
Hata hivyo aliomba mradi huo upanuliwe ili kukidhi ongezeko la wakazi wa Ikwiriri ambalo limefikia wananchi 45,000.
Ziara ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji inaendelea leo katika mkoa wa Lindi ambapo itakagua miradi ya maji iliyopo Rombomnara na Ng’apa iliyopo mkoani humo.

No comments:
Post a Comment