SKYLIGHT BAND YAIBUA KIFAA KIPYA MITHILI YA KASUKU SI MWINGINE NI ASHURA KITENGE, NJOO LEO UMSHUHUDIE LIVE THAI VILLAGE
Mratibu wa Skylight Band, Lubea akimkaribisha mdau wa bendi hiyo Miryam Kamaliza shot ya Tequila wakati wa show iliyobamba wakazi wa Dar Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki.
Mratibu wa Skylight Band, Lubea akimimina kinywaji cha Tequila kwa Meneja wa Skylight Band, Aneth Kushaba AK47 Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village.
Meneja wa Skylight Band, Aneth Kushaba AK47 akipiga kilaji cha Tequila kupasha mwili joto kabla ya kupanda jukwaani, kinywaji hicho ni maalum kwa mashabiki wa bendi hiyo pindi wanapoingia kwenye kizingiti cha ukumbi huo wa Thai Village, Masaki jijini Dar.
Msanii wa Skylight Band Joniko Music (katikati), akifungua dimba la burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo huku akipewa sapoti na Aneth Kushaba AK 47 pamoja na Sam Mapenzi (kulia) wakati show zao za kila Ijumaa ndani ukumbi wa Thai Village Masaki, jijini Dar.
Aaaah Komando Kipensi weeeeeee… si mwingine ni Le Manager her self Aneth Kushaba AK 47 mutoto ya Kisukuma akifanya yake jukwaani Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar……Tukutane baadae pale kati….Full MAU-KODAK kuwa huru kuomba picha na washikaji zako mdau wetu.
Murembo mupya binti mwenye sauti ya kumtoa Nyoka pangoni, Ashura Kitenge akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar es Salaam Ijumaa iliyopita huku akipewa sapoti na Rapa mkongwe Joniko Flower pamoja na Aneth Kushaba AK47.
Mashabiki wa Skylight Band wakijimwaga kwa raha zao.
Meneja wa Skylight Band, Aneth Kushaba AK47 a.k.a #KomandoKipensi akiwa kwenye hisia kali wakati akitoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo (hawapo pichani) Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar.
Sam Mapenzi akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) huku akipewa sapoti ya back vocal na Rapa Joniko Flower pamoja na Sony Masamba.
Daudi Tumba akifanya yake jukwaani kuhakikisha mashabiki wa Skylight Band wanapata ladha nzuri ya muziki wa Live ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar Ijumaa iliyopita.
Comments