KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA ASHIRIKI KUPANDA ZAO LA MWANI BAHARINI

1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa jimbo la  Muyuni Mh. Mahadhi Juma Mahadhi wakati alipowasili katika tawi la Pete ambapo amezungumza na wajumbe wa halmashauri ya wilaya ya Kusini akisisitiza zaidi masuala ya kushughulikia matatizo ya wananchi na kuwa waadilifu ili wananchi wawaamini katika majukumu yao jambo ambalo litakifanya Chama cha Mapinduzi kuaminika zaidi na wananchi kwani chama hicho ni kikubwa na kina historia kubwa kwa upande wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,ambapo pia Katibu mkuu huyo  anahamasisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya  mwaka 2010 ,  Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Kinana anaongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Katikati ni Mwakilishi wa jimbo la Muyuni Mh. Jaku Hashim.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA  FULLSHANGWE-MAKUNDUCHI- UNGUJA KUSINI)2Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana Samia Suluhu Mbunge wa jimbo la Makunduchi mara baada ya kuwasili katika tawi la Pete Makunduchi, katikati ni Mwakilishi wa jimbo la Makunduchi Haroun Ali Suleiman.3Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mh. Wanu Hafidh Ameir Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Mwakilishi nafasi za vijana  4Mh. Wanu Hafidh Ameir Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Mwakilishi nafasi za vijana  kushoto pamoja na wajumbe wengine wakiwa katika mkutano wa ndani wakati Katibu Mkuu Kinana akiwasili ukumbini hapo.5Kutoka kulia ni Mwakilishi wa jimbo la Makunduchi Haroun Ali Suleiman. Mbunge wa jimbo la Makunduchi Samia Suluhu na Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg. Sauda Mpambalyoto 7Baadhi ya wajumbe wakiwa katika mkutano huo.8Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya Kusini mkoa wa kusini Unguja9Baadhi ya watalii nao wakavutiwa na ziara ya katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na kujichanganya na wana CCM  katika ziara hiyo.10Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa taifa katika ofizi ya jimbo la Muyuni pamoja na Mbunge wa jimbo hilo Mahadhi Juma Mahadhi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.12Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimjulia hali Mzee Ali Haji ali  Mwenyekiti mstaafu wa CCM wilaya ya Kusini wakati alipofika nyumbani kwake katika kijiji cha Kibigija.13Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangwe Bw. John Bukuku kushoto na Mkurugenzi wa Mawasiliano CCM Bw. Daniel Chongolo katikati wakipata picha ya pamoja na watalii katika ufukwe  wa Kibigija wakati Katibu Mkuu wa CCM alipotemelea kilimo cha Mwani kijijini hapo.14Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akielekezwa njia ya kupita na Mwakilishi wa jimbo la Muyuni Mh. Jaku Hashim wakati alipotembelea kikundi cha akina mama wanaojishughulisha na kilimo cha Mwani baharini.15Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na Mwakilishi wa jimbo la Muyuni Mh. Jaku Hashim wakishiriki kupanda zao la Mwani baharini.16Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na Mwakilishi wa jimbo la Muyuni Mh. Jaku Hashim wakishiriki kubuna zao la Mwani baharini.1718Mmoja wa akina mama wanaojisshughulisha na kilimo hicho akitoa maelezo kwa waandishi wa habari.19Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kubeba mawe katika ujenzi wa ofisi ya CCM tawi la Kiunga Mtende jimbo la Muyuni.22Mbunge wa jimbo la Makunduchi Samia Suluhu akizungumza wakati akizungumza neno wakati wa kuweka jiwe la msingi katika jengo la ukumbi wa mikutano wa ofisi ya wilaya ya Kusini.23Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi katika ukumbi wa ofisi ya  CCM wilaya ya Kusini kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi Mh. Mwakilishi wa jimbo la Makunduchi Haroun Ali Suleiman.W1Baadhi ya wana CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara huyu alikuwa amevaa miwani ikionyesha mwaka 2015 kama ishara ya mwaka muhimu wa Uchaguzi na kura ya Maoni ya Katiba mpya inayopendekezwa.W2Mbunge wa jimbo la Makunduchi Mh. Samia Suluhu akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kizimkazi Mkunguni Makunduchi.W3Umati wa watu waliohudhuria katika mkutano huo.W4W5Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Kizimkazi Mkunguni jimbo la makunduchi.W6Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kizimkazi Mkunguni jimbo la MakunduchiW7W8Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiakikabidhi majiko kwa vikundi vya akina mama wa makunduchi yaliyotolewa na Mbunge wa jimbo la Makunduchi Mh. Samia Suluhu  na  Mh. Mwakilishi wa jimbo la Makunduchi Haroun Ali Suleiman.W9Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi pikipiki za matairi matatu na za matairi mawili kwa vikundi vya mazingira zilizotolewa na Mbunge wa jimbo la Makunduchi Mh. Samia Suluhu  na Mh. Mwakilishi wa jimbo la Makunduchi Haroun Ali Suleiman.

Comments