Wednesday, January 28, 2015

ZIARA YA DG WA NHC KATIKA MIKOA YALETA MATUMAINI KWA VIJANA

 
 Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu wakikagua eneo lililotengwa kwa ajili ya NHC kujenga  nyumba za gharama nafuukatika Halmashauri ya Wilaya Serengeti-Mugumu. Eneo hili lina ekari 134 na miundombinu ya maji na umeme.

 Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mugumu Serengeti akimuonyesha Mkurugenzi Mkuu wa NHC ramani ya mpango Miji inayoonyesha eneo la NHC la kujenga nyumba za gharama nafuu.

 Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akiongea na kikundi cha vijana Wilayani Serengeti waliyosaidiwa mashine na NHC kwa ajili ya kujiajiri kupitia utengenezaji wa matofali yanayofungamana

 Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake wakikagua jengo la biashara lililojengwa na NHC eneo la Mukendo Musoma.

 
 Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akitoa maelekezo ya matumizi bora ya dari la jengo la biashara la Mukendo lililojengwa na NHC katika Manispaa ya Musoma ili kuongeza mapato ya Shirika.


Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake walipotembelea Wilayani Tarime kujionea nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC mwaka 1968 na ambazo hadi hivi sasa zinasaidia familia mbalimbali. Nyumba hizi ni za vyumba viwili na zilipewa  Halmashauri hiyo mwaka 1991.

Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akijadili namna ya kuongeza ubora wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini. Amesisitiza kupunguza gharama ya ujenzi ili nyumba zinazojengwa ziwe nafuu.

 

 Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukiangalia mnara wa kumbukumbu ya mahali ambapo ilikuwepo nyumba aliyozaliwa Baba wa Taifa.

 
 Mojawapo ya nyumba aliyoishi Mwalimu Nyerere ambayo ilijengwa 1974 na aliyekuwa Rais wa Msumbiji Hayati Samora Moses Machel.

 
 Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu aliwa amekaa sehemu maarufu aliyokuwa akikaa Mwalimu Nyerere wakati wa kucheza bao.

New Picture (13)Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la Isibania nchini Kenya kujionea namna nchi hiyo ilivyopanga eneo lao la mpakani.

New Picture (14)Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la Sirari kuona eneo la kujenga nyumba ili kuboresha taswira ya mpaka wa nchi yetu. Ujumbuliongozwa na Maafisa Ardhi wa Wilaya ya Tarime.
New Picture (15)Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake pamoja naongozi wa Wilaya ya Butiama wakikagua eneo lililotengwa na Wilaya hiyo ili NHC ijenge nyumba za gharama nafuu. Bw. Mchechu amesisitiza kuwa NHC itajenga nyumba katika Wilaya hiyo ili kuenzi mchango wa Mwalimu Nyerere wa kulianzisha Shirika la Nyumba la kwanza nchini Tanzania mwaka mmoja tu baada ya uhuru.

No comments: