Wednesday, January 28, 2015

DHARUBA KUBWA YA THELUJI NA UPEPO MKALI IMEIPELEKEA KUSIMAMISHA HUDUMA ZA UMMA KASKAZINI MASHARIKI YA MAREKANI.

By Abou Shatry Washington DC
Zaidi ya watu 60 million wataathirika kutokana na kimbunga kikubwa cha upepo unaoambatana na unyeshaji wa theleji katika eneo la kaskazini mashariki ya Marekani.
A plow truck clears snow off South Church Street, in Hazleton, Pennsylvania on Monday. The area received another three-inches of snow overnight
Lori maalumu la usafishaji likiondoa theluji iliondoka barabara ya South Church Street, katika mji wa Hazleton, Pennsylvania siku ya Jumatatu Jan 26, 2015. Photo via .dailymail.co.uk
Kwa mujibu wa kitengo cha hali ya hewa nchini Marekani, imetaja maeneo ambayo yataathiriwa na dhoruba hiyo, ya kihistoria ambayo itapelekea zaidi ya watu kadhaa kukosa huduma ya umeme, pamoja na huduma za usafiri wa anga na nchi kavu.
 
Imetaja baadhi ya majimbo ambayo yatakumbwa na kimbunga hicho kuwa ni New York, New Jersey, Massachusetts, Connecticut na Rhode Island, ambapo imepelekea viongozi wakuu wa majimbo hayo kutangaza hali ya hatari kwa tukio hilo ambalo litatokea siku ya Jumatatu, Jumanne na Jumatano.
 
Imetabiriwa kiasi cha unyeshaji wa theluji hiyo 36inches katika jimbo la New York 16 hadi 26 inches katika jimbo la Boston, na kiwango kingine kama hicho katika baadhi ya majimbo mengine
 
Zaidi ya safari za ndege 3,800 zimesimamishwa mapema leo Jumaatatu katika viwavya vya ndege vya JFK, LaGuardia na Newark airports, pia huduma za shule kufungwa siku ya jumanne na jumatano katika majimbo hayo.
Chanzo: swahilivilla 

No comments: