Friday, January 23, 2015

WAZIRI SAADA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KARIAKOO NA MTAA WA NAMANGA

unnamed (39). Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (wa pili kulia) akiongoza na viongozi wa mkoa wa kodi wa Ilala kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na maafisa wa Serikali alipofanya ziara ya kushtukiza jana jijini Dar es salaam katika soko la Kariakoo kujionea namna wafanyabiashara wanavyozingatia na kusimamia matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD ambazo wanazopaswa kuzitumia mara wanapouza bidhaa zao ili kusaidia Serikali kukusanya mapato na kuboresha utoaji wa huduma za jamii nchini. Wa kwanza kulia ni Kaimu Msaidizi wa Meneja wa mkoa wa kodi wa Ilala kutoka TRA Hamidu Athmani, wa kwanza kushoto ni Kaimu Meneja wa mkoa wa kodi wa Ilala Elias Balongo na kushoto mwa Waziri ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda. unnamed (40)Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda (wa kwanza kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (wa pili kushoto) katika ziara ya kushtukiza katika soko la Kariakoo kujionea namna wafanyabiashara wanavyozingatia na kusimamia matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD ambazo wanazopaswa kuzitumia mara wanapouza bidhaa zao ili kusaidia Serikali kukusanya mapato na kuboresha utoaji wa huduma za jamii nchini. Aliyevaa tai kulia ni wa kwanza kulia ni Kaimu Msaidizi wa Meneja wa mkoa wa kodi wa Ilala kutoka TRA Hamidu Athmani.
unnamed (41)Wananchi wakifuatilia ziara ya kushtukiza ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum aliyofanya jana jijini Dar es salaam katika soko la Kariakoo kujionea namna wafanyabiashara wanavyozingatia na kusimamia matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD ambazo wanazopaswa kuzitumia mara wanapouza bidhaa zao ili kusaidia Serikali kukusanya mapato na kuboresha utoaji wa huduma za jamii nchini.
(Picha na Eleuteri Mangi- MAELEZO)
……………………………………………………………………….
NA Eleuteri Mangi- MAELEZO
Uelimishwaji bado unahitajika kwa wafanya biashara nchini katika na kuhakikisha wazingatia na kusimamia matumizi sahihi ya mashine za kielektroniki za EFD.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum alipofanya ziara ya kushtukiza katika soko la Kariakoo kujionea namna wafanyabiashara wanavyozingatia na kusimamia matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD ambazo wanazopaswa kuzitumia mara wanapouza bidhaa zao ili kusaidia Serikali kukusanya mapato na kuboresha utoaji wa huduma za jamii nchini.
“Nasisitiza wafanyabiashara wote nchini kutumia mashine za kielektroniki za EFD katika biashara zao, niwaombe muwe na mwamko wa ulipaji kodi kwa maendeleo ya nchi yetu ” alisema Waziri Saada.
Zaidi nya hayo, Waziri amesisitiza kuwa wafanyabiashara wajisajili katika mfumo wa VAT ili kuokoa mapato yanayopotea ambapo ameeleza kuwa nchi zilizoendelea wanatoa misaada kwa nchi zinazoendelea kutokana na makusanyo ya wananchi wa nchi hizo kujali na kuthamini kulipa kodi kutoka wafanyabiashara na watumishi wengine.
Pia Waziri Saada aliuagiza uongozi wa TRA kuwa karibu na wafanyabiashara kwa naq kutoa namba zao za simu ili wateja waweze kuwasiliana nao mara mashine zao zinapokuwa na hitilafu na kutoa taarifa kwa haraka badala na kuwa na ufanisi wa haraka nan wenye tija kwa taifa. 
Naye Kaimu Meneja wa mkoa wa kodi wa Ilala kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Elias Balongo amesema kuwa wataendelea kutoa elimu kwa wananchi wote kutambua umuhimu wa kudai risiti baada ya kununua bidhaa na kwa wafanyabiashsra kutoa risiti baada ya kuuza bidhaa.
Kwa upande wake mfanyabiashara wa Namanga jijini Dar es salaam Saleh Kassim Seif alisema kuwa wanaishukuru Serikali kuanzisha mfumo wa matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD kwani unamanufaa kwao ambapo unawasaidia kujua mauzo yao ya siku, wiki, mwezi hadi mwaka ili ambapo wameweza kuboresha bishara zao kwa kuwa na kumbukumbu sahihi ya mauzo yao.
Aidha, mfanyabiashara huyo alisema kuwa wanapata changamoto ya mashine hizo kuharibika wanaomba zitengenezwe ndani ya saa 24 ili waweze kutoa huduma yenye kuzingatia sheria, kanuni na taraibu za buiashara nchini.
Katika ziara hiyo, Waziri wa Fedha aliandamana viongozi wa wa mkoa wa kodi wa Ilala kutoka TRA, waandishi wa habari na baadhi ya maafisa wa saerikali.

No comments: