Friday, April 11, 2014

WANANCHI WASISITIZWA KUWEKEZA KATIKA MIRADI YA GESI NCHINI

Mwandishi wa kitabu kinachoelezea namna watanzania na makampuni ya usambazaji ya hapa Tanzania yanavyoweza kushiriki, kuwezeshwa na kunufaika na sekta ya nishati ya gesi asilia hapa.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo  Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akiteta Jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue jana wakati wa uzindizi wa kitabu cha “Local Content in…
Mwandishi wa kitabu kinachoelezea namna watanzania na makampuni ya usambazaji ya hapa Tanzania yanavyoweza kushiriki, kuwezeshwa na kunufaika na sekta ya nishati ya gesi asilia hapa.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo  Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akiteta Jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue jana wakati wa uzindizi wa kitabu cha “Local Content in Supplier Development” kilichoandikwa na Neema Lugangilra Apson.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto), Bi. Neema Lugangilra Apson (katikati) na Balozi wa Uingereza Dianna Melrose wakimsikiliza mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi huo jana usiku jijini Dar es salaam.
Mgeni Rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu kinachoeleza namna watanzania na makampuni ya usambazaji yanavyoweza kushiriki, kuwezeshwa na kunufaika na sekta ya nishati ya gesi asilia hapa. Kulia ni mwandishi wa kitabu hicho Bi. Neema Lugangilra Apson.
Bi. Neema Lugangilra Apson akionesha kitabu chake kinachoitwa “Local Content in Supplier Development” kinachoelezea namna watanzania na makampuni ya usambazaji yanavyoweza kushiriki, kuwezeshwa na kunufaika na sekta ya nishati ya gesi asilia hapa.
Mgeni Rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipokea kitabu kinachoelezea namna watanzania wanavyoweza kushiriki na kunufaika na sekta ya nishati ya gesi asilia hapa nchini. Kulia ni mwandishi wa kitabu hicho Bi. Neema Lugangilra Apson.
Bi. Neema Lugangilra Apson akimkabidhi Binti yake Georgia Blessings Apson  kitabu alichokiandika kinachoelezea namna watanzania na makampuni ya usambazaji yanavyoweza kushiriki, kuwezeshwa na kunufaika na sekta ya nishati ya gesi asilia hapa.
Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Assah Mwambene (katikati) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Local Content in Supplier Development kilichoandikwa na Bi. Neema Lugangilra Apson jana Jijini Dar es Salaam, kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN) Gabriel Nderumaki.
SERIKALI imewasisitiza wananchi hususan wafanyabiashara kote nchini kuwekeza katika utoaji wa huduma  mbalimbali za kijamii  katika maeneo yote yenye miradi ya gesi nchini.
Kauli hiyo imetolewa  jana usiku jijini Dar es salaam  na  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu kilichoandikwa na mtanzania Bi. Neema Lugangira Apson chenye  maudhui ya namna Kampuni za Kitanzania zilizojikita katika uwekezaji wa gesi zinavyoweza kushiriki ,kuendelezwa katika uwekezaji wa sekta ya gesi asilia nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, balozi, makampuni yaliyowekeza katika sekta ya gesi na wadau mbalimbali Balozi Sefue amesema sekta ya gesi ni moja eneo lililo na fursa nyingi za uwekezaji kwa watanzania.
Amesema ni wakati wa wananchi kuziona fursa hizo na kuwekeza katika maeneo yote yanayohitaji uwekezaji wa huduma mbalimbali hususan za usambazaji  na uuzaji wa vyakula, ujenzi wa nyumba za kulala wageni, uuzaji wa bidhaa muhimu, uuzaji wa bidhaa na vifaa vya  gesi pamoja na vitu vingine vinavyohitajika katika maeneo ya miradi.
Ameeleza kuwa serikali imejipanga vizuri katika kuhakikisha kuwa sekta ya gesi inasimamiwa na kuendelezwa vizuri kisera na kufafanua kuwa tayari hatua mbalimbali zimekwisha chukuliwa kuhakikisha kuwa sekta ya gesi inakuwa na manufaa kwa wananchi na ustawi wa taifa.
“Katika hili serikali tumejipanga vizuri kwa kuhakikisha sekta hii inaleta manufaa kwa taifa, tumejifunza kupitia uzoefu mkubwa walioupata wenzetu  hasa nchi kubwa zilizopiga hatua katika sekta ya gesi” Amesisitiza Balozi Sefue.
Balozi Sefue amewataka wafanyabiashara na wasambazaji wa ndani walioingia kwenye sekta ya nishati ya gesi na mafuta  kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa  na kuzingatia ubora na viwango vinavyokubalika ndani na nje ya nchi na kuwasisitiza kuendelea kujifunza zaidi na kutafuta masoko ya bidhaa wanazozalisha ili kujenga uchumi imara.
Amesema serikali inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wanaowekeza katika sekta ya gesi na utafutaji wa mafuta nchini na kutoa wito kwa makampuni yanayojihusisha na sekta ya gesi kushirikiana na serikali katika mpango wa kuhakikisha shughuli wanazozifanya zinaboresha maisha ya watanzania.
Akizungumzia uzinduzi wa kitabu hicho Balozi Sefue amesema kuwa kitabu hicho kina mchango muhimu sana katika uendelezaji wa sekta ya gesi hapa nchini na kufafanua kuwa elimu iliyomo ndani ya kitabu hicho ni kwa manufaa ya watanzania wote.
Picha/Habari   na Aron Msigwa na Eliphace Marwa – MAELEZO.

No comments: