Friday, April 11, 2014

Timu ya watoto wa mitaani ya jijini Mwanza Yarejea Nchini na Kombe la Dunia Katika Mchezo wa Soka

  Mchezaji aliyesabibisha timu ya watoto wa mitaani kutoka Tanzania kuibuka mabingwa wa Dunia kwa kufunga magoli 3-1 dhidi ya Burundi Frank William (mwenye kofia nyekundu) akiwa na baadhi ya wachezaji wenzake mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jana. Kushoto ni Hassan Jaffar,Emmanuel Amos, na Hassan Seleman.
 Mwenyekiti wa Timu ya watoto wa mitaani ya jijini Mwanza Alfat Mansoor (Dogo) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya timu hiyo kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Frank Shija akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa timu ya watoto wa mitaani.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Bi. Juliana Yassoda akiwa amebeba kombe la ubingwa dunia mara baada ya kuwapokea wachezaji wa timu ya watoto wa mitaani ya Tanzania iliyochukua ubingwa huo kwa kuifunga timu kutoka Burundi jumla ya magoli 3-0. Timu hiyo imewasili nchini jana majira ya saa 9:35 mchana na kulakiwa na uongozi wa Serikali na wadau mbalimbali wa soka.
 Wachezaji wa timu ya watoto wa mitaani ya Tanzania ilyo nyakuwa ubingwa wa dunia katika mashindano yaliyofanyika nchini Brazil kwa kushirikisha timu za watoto wa mitaani, wakiwa wamebeba makombe waliyoyapa katika mashindano hayoPicha zote na Frank Shija, Afisa Mawasiliano Serikalini- Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

No comments: