Rais wa Zanzibar Dk Ali Shein Akutana na Uongozi wa Wizara ya Habari,utalii,Utamaduni na Michezo Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Habari,utalii,Utamaduni na Michezo, katika kikao cha utekelezaji Mpango kazi kwa kipindi cha Julai hadi Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar jioni jana,
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo, Dkt. Ali Mwinyikai,akiwasilisha mpango wa utekelezaji wa mpamgo wa kazi wa Wizara hiyo katika kipindi cha robo mwaka kutoka Julai -Machi 2013/2014,katika kikao kilichofanyika jana jioni ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar, chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi (kushoto).Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar
Comments