Posted by
Vempin Media Tanzania
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mfanyakazi wa Kampuni ya Dira, Ally Makuburi akimjulia hali Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Bw. Alex Msama ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kulia ni Musa Mkama mwandishi wa gazeti hilo pia.
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam inayoandaa matamasha ya Pasaka na Krismwas, Bw. Alex Msama anaendelea vizuri baada ya kupata ajali mkoani Dodoma kisha kupelekwa katika hospitali ya mkoa wa Dodoma na baadaye kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika wodi ya Kibasila namba 16 hivi sasa anaendelea vizuri na amesema hali yake imekuwa ikiimarika tofauti na ilivyokuwa mwanzo. Aliiambia Fullshangwe jana hospitalini hapo kwamba Mungu ni mwema na ametenda miujiza yake ndiyo maana amekuwa akiimarika kiafya.
Mfanyakazi wa Kampuni ya Dira, Musa Mkama, akimjulia hali Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Alex Msama ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kupata ajali mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion, Bw. Alex Msama, akiwa na wafanyakazi wake na baadhi ya ndugu na jamaa wakati walipokwenda kumjulia hali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jana.
Comments