Tanzania @ 50 Wimbo Maalumu wa Muungano Utanzania Wetu ni Muungano Wetu, Tuulinde, Tuudumishe na Tuuimarishe
Wimbo: TUULINDE
Watunzi: LAMECK DITTO, AMINI MWINYIMKUU
Watayarishaji: EMA THE BOY, TUDDY THOMAS
Studio: SURROUND SOUND
Wasifu wa Wimbo: Wimbo huu maalumu wa Muungano umeimbwa na wasanii 50, kutoka katika mahadhi tofauti tofauti ya muziki kama Bongo Flava, Taarab, Dansi, Hiphop na muziki wa injili. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, wasanii 50 tofauti kuimba wimbo kwa pamoja, na kwa ushirikiano mkubwa, wasanii hawa wanatukumbusha umuhimu wa Muungano ambao ndio utanzania wetu.
Baadhi ya Wasanii waliohusika Amini Kadjanito Mwasiti Linah Christina Shusho Khadija Kopa Frola Mbasha Ommy Dimpoz Diamond Josse Mara Kalala Jr Ali Kiba Peter Msechu Mrisho Mpoto Abdul Kiba Mzee Yusuph Angel Mwana Fa Nikki Wa pili G Nako God Zilla Madee Asley Shaa Mandojo Domokaya Shilole
Comments