Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya Atangaza Rasmi Kung’atuka Nafasi Zote Za Uongozi Baada ya Kuitumikia Serikali na Chama Cha Mapinduzi(CCM)Kwa Zaidi ya Miaka 33
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Waziri mkuu Mstaafu mzee Cleopa David Msuya aliyetangaza rasmi kung’atuka nafasi zote za uongozi baada ya kuitumikia serikali na Chama Cha Mapinduzi(CCM) kwa zaidi ya miaka 33. Mzee Msuya alitangaza hayo katika hafla maalumu iliyofanyika katika ofisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi wilayani Mwanga
Wazee wa wilaya ya Mwanga wakimkabidhi Mzee Cleopa David Msuya zawadi mbalimbali na kumkaribisha kijijini wakati wa hafla ya kumuaga kama kiongozi iliyofanyika katika ofisi kuu ya CCM Wilayani Mwanga jana
Waziri Mkuu Mstaafu mzee Cleopa David Msuya akitoa hotuba yake mjini Mwanga jana wakati wa hafla ya kumuaga baada ya utumishi wa umma wa muda mrefu.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza na kuzungumza na Waziri mkuu Mstaafu mzee Cleopa David Msuya aliyetangaza rasmi kung’atuka nafasi zote za uongozi baada ya kuitumikia serikali na Chama Cha Mapinduzi(CCM) kwa zaidi ya miaka 33. Mzee Msuya alitangaza hayo katika hafla maalumu iliyofanyika katika ofisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi wilayani Mwanga
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri Mkuu mstaafu Mzee Cleopa David Msuya wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika ofisi kuu ya CCM mjini Mwanga, Mkoani Kilimanjaro jana ambapo Mzee Msuya alitangaza kung’atuka rasmi kutoka nafasi zake zote za uongozi wa umma.Wengine katika picha walioketi mbele kutoka kushoto ni Mkuu wa mkoa wa KilimanjaroBwana Leonidas Gama, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, na kulia ni Waziri wa maji mbaue pia ni mbunge wa Mwanga Profesa Jumanne Maghembe. Picha na Freddy Maro IKULU
Comments