Makamu
wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilali ametembelea
viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kujionea maonesho ya Miaka
50 ya Muungano yanayoendelea katika vuiwanja hivyo. Miongoni mwa mabanda
aliyotembelea ni banda la Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
(HESLB) na pichani ni Makamu wa Rais akikaribishwa bandano hapo na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Asangye Bangu.
Makamu
wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilali akisalimiana na watumishi wa HESLB
mara baada ya kufika bandani haopo na kupokea maelezo ya shughuli za
HESLB ikiwa ni mafanikio, matarajio na changamoto mbalimbali
zinazowakabili na jinsi wanavyo jitahidi kukabiliana nazo.
Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Asangye Bangu akitoa maelezo kwa Makamu
wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilali juu ya shughuli za bodi wakati
alipotembelea banda la Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
(HESLB) lililopo katika viwanja vya Mnazi mmoja yanapofanyika maonesho
ya Miaka 50 ya Muuungano Dar es Salaam.
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilali akitoa neno wakati alipotembelea banda hilo.
Baadhi
ya watumishi wa Bodi ya Mikopo wakiwa bandani hapo kusubiri wananchi
wawape maelezo ya shughuli zao na nini mtu akifanye apate mkopo.
Comments